Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda (wa pili kulia) Makamu wa Rais na Mkuu wa eneo la Biashara wa Afrika Mashariki, Adam Jones (wa pili kushoto) kwa pamoja wakionesha bango la mfano wa Master Card, wakati wakizindua rasmi huduma ya Airtel Money Master Card, huduma itakayomuwezesha mteja wa mtandao huo, kufanya malipo kidigitali kwa urahisi na kwa usalama zaidi. Hafla fupi ya uzinduzi huo imefanyika mchana huu katika Ofisi za Airtel zilizopo Moroco jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji (kushoto) ni Mkurugenzi wa Master Card Afrika Mashariki, Frank Molla.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (kulia|) akifafanua jambo kuhusu kadi hiyo ya Master Card wakati wa hafla ya uzinduzi.
Wakipongezana baada ya kuzindua rasmi.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akifafanua jambo kuhusu huduma mpya ya Airtel Money Master Card, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ofisi za Airtel mchana huu.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Master Card, huduma ambayo itamwezesha mteja wa mtandao huo kufanya malipo ya kidigitali kwa urahisi na salama zaidi. Kushoto ni Makamu wa Rais na Mkuu wa eneo la Biashara wa Afrika Mashariki, Adam Jones (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakifuatilia kilichokuwa kikiwasilishwa na viongozi wao.
Makamu wa Rais na Mkuu wa eneo la Biashara wa Afrika Mashariki, Adam Jones, akizungumza.
Mkurugenzi wa Master Card Afrika Mashariki, Frank Molla (katikati) akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji, akizungumza.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano,
akifafanua jambo jinsi ya kutengeneza Master Card kupitia simu ya mkononi.
Meneja wa Airtel Money Master Card, Nassor Abubakar, akifafanua jambo kuhusu matumizi ya kadi hiyo.
Mwanahabari wa kwanza kujiunga na huduma hiyo, James, akielezea faida na jinsi alivyosukumwa kujiunga kwa haraka.
No comments:
Post a Comment