Msanii mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya, Ally Kiba, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, kuhusu mipango yake ya kazi anazotarajia kuanza hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 17 tangu alipoanza kazi ya sanaa.
*****************************************
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ali Saleh Kiba 'Ali Kiba' ametangaza kuwa baada ya kutimiza miaka 17 katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya ameandaa ziara maalumu katika mikoa mbalimbali ambapo atajumuika na maashabiki wake katika mchezo wa Soka na kupima afya ziara ambayo, itakayoitwa 'Ali Kiba Unforgetable tour'.
Akizungumza na wanahabari Kiba, alisema ziara hiyo ni sehemu ya kutoa shukrani kwa washabiki wake kwa sapoti waliompa tangu alipoanza tasnia hiyo.
Aidha alisema kuwa katika ziara yake hiyo atafanya mambo makubwa matatu ambayo ni kutembelea wanafunzi wa elimu ya juu mikoa mbalimbali nchini, kutoa huduma za afya bila malipo katika mikoa hiyo atakayotembelea pamoja na kushindanisha soka na baadae shoo itakayohusisha wasanii wa Kings Music Record na wengine watakaoungana nae.
Kiba alisema katika ziara kwa wanafunzi wa elimu ya juu amepanga kuzungumza nao juu ya mbinu za kujikwamua kimaisha mbali na kutegemea kuajiriwa.
Kuhusu huduma za bure za afya alisema atatumia wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Muhimbili na Mloganzila pamoja na ya mkoa husika kutoa huduma hizo kwa wananchi wa eneo husika watakaokwenda kupima afya zao, kupatiwa matibabu pamoja na kuelimishwa juu ya ugonjwa wa ebola.
Pia alisema kwa upande wa mashindano ya soka atashindanisha timu ya mkoa husika na atakayoichagua yeye huku akiwa kocha wa timu hiyo kisha baadae itafanyika shoo itakayohusisha wasanii mbalimbali wakiwemo wa Kings Music Record.
Aidha Ali Kiba, alitumia wakati huo kumtambulisha msanii wake mpya katika lebo yake aliyemtambulisha kwa jina la Tommy Fleva.
Sehemu ya wanahabari waliohudhuria katika mkutano huo wa tamko la King Kiba.
No comments:
Post a Comment