Habari za Punde

MAZIWA YA KOPO SASA BASI, YATAJWA NI HATARI KWA AFYA YA MTOTO

MAWAZIRI was nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC wanaoshughulukia masuala ya Afya, VVU, na UKIMWI kwa pamoja wamepitisha katazo la Matangazo ya Maziwa ya KOPO ili kutia msisitizo kwa kinamama kuwanyonyesha watoto wao kuanzia miezi sita Hadi miaka miwili ili kupunguza Viribatumbo.
"Lishe bado ni tatizo kubwa katika nchi wanachama was SADC pamoja na Mambo mengine ya huduma za lishe katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika na tumekubaliana na kupitisha maazimio ya matumizi ya kadi alama za lishe kwa nchi za SADC". alisema Waziri Ummy.
Aidha alisema kuwa nchi wanachama wa SADC wamejiwekea kanuni za pamoja za katazo giko la uhamasishaji wa matumizi ya Maziwa ya kopo na vyakula vya mbadala kwa watoto wachanga na wadogo na kumlinda mama anayenyonyesha (yaani likizo ya uzazi).
"Katika kikao chetu pia tumekubaliana kutumia mfumo wa kikanda wa kuboresha Lishe kwa watoto na mkakati wa kikanda wa kudhibiti uzito uliozidi na kilibatumbo  katika Jamii,
Uongezwaji wa virutubishi vya vitamini na madini wakati wa usindikaji kwenye unga wa Mahindi, unga wa ngano, sukari na mafuta ya Kula na chumvi .alisema Waziri Ummy.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Affya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu, wakati akitoa majumuisho ya kikao Cha Cha Mwaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC wanaoshughulikia masuala ya Afya waliokutana jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu lishe na Afya hususan magonjwa ya Kifua Kikuu, Maralia, VVU na UKIMWI.
Waziri Ummy alisema kuwa pamoja na Mambo mengine katika mkutano huo wameazimia kuwa katika nchi za Ukanda was SADC Zina changamoto ya kuwa na wagonjwa wengi wankifua Kikuu sugu ambapo katika nchi za SADC zinachangia jumla ya asilimia 77 ya wagonjwa hao katika bara la Afrika.
Aidha alisema kuwa kufuatia changamoto hiyo, Nchi  wanachama wamepitisha mpango mkakati was kudhibiti Kifua Kikuu katika nchi wanachama was SADC ifikapo 2020-2025.
Katika kikao hicho Mawaziri walipitisha maazimio ya kutokomeza Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030, kushirikiana na kuoanisha  Sera na Miongozo ya kitaifa ya kudhibiti TB katika Ukanda wa SADC ili kuboresha huduma za Kifua Kikuu.
Maazimio mengine ni pamoja na kuimarisha ushirikiano Kati ya mipango ya Kifua kikuu na UKIMWI, Sekta binafsi, Asasi za kiraia na Sekta zingine katika Ukanda wa SADC, Kuimarisha udhibiti wa Kifua Kikuu katika maeneo ya Migodi hasa wachimbaji wa madini katika maeneo ya mipakani kwa kuboresha mifumo ya utoaji wa taarifa na rufaa za wagonjwa wa Kifua Kikuu baina ya nchi wanachama.
Waziri Ummy alisema kuwa katika nchi za SADC Virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI vimeendelea kuwa changamoto kubwa na kupitia maazimio ya kuweka kioaumbele katika kutoa huduma za unasihi na kupima VVU kwa makundi yaliyoko katika hatari kubwa ya maambukizi ya VVU wakiwemo vijana balehe wa kike na kina mama wadogo.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa nchi wanachama was SADC watajikita katika matumizi ya dawa ili kufikia malengo ya 90:90:90 ya kuutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.
Kwa upande wa Maralia Waziri Ummy, alisema kuwa kutikana na upgonjwa wa Maralia kuendelea kuwa tishio kwa Afya za wananchi wa nchi za SADC, wamepitisha maazimio ya kuendelea kufuatilia ubora wa dawa za kutibu Maralia na kuendelea kufanya utafiti wa usugu wa vimelea vya Maralia dhidi ya dawa zinazotumika.
"Tutaendeleza ushirikiano wa mapambano dhidi ya Maralia katika nchi za SADC kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na mikakati iliyoandaliwa kwa kushirikiana baina ya Program za Maralia za nchi wanachama (Cross border collaboration),
Pia tunaendelea kufuatilia ubora wa viuatilifu vinavyotumika kwenye afua za vyandarua na dawa ,ukoko ili kuona kama vinaendelea kuwa na ubora unaotakiwa katika kudhibiti mbu na kuendelea  na utafiti ili kubaini maeneo yenye maambukizi makubwa ya Maralia na kuchukua hatua za kudhibiti". alisema Waziri Ummy
Kwa upande wa Maafa na dharura Waziri Ummy, alisema kuwa Maafa na magonjwa ya mlipumo yamekuwa tishio katika nchi ya SADC na hasa ugonjwa wa EBORA, ambapo wamepitisha maazimio ya kuanzisha kikosi kazi cha nchi wanachama was SADC cha uratibu wa pamoja katika kushughulikia ugonjwa wa EBORA Afrika.
Maazimio mengine ni kuboresha mafunzo kuhusu masuala ya Maafa na dharura, kushirikiana katika maandalizi na mwitikio wa dharura ikiwemo kuwajengea uwezo watoa huduma katika maeneo ya mipakani na kupeana taarifa kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.