Habari za Punde

MKUTANO MKUU WA 18 WA NCHI ZA AFRIKA NA NURDIC KUFANYIKA DAR ES SALAAM NOV 8

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Faraji Mnyepe, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, jana kuhusu ujio wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Nchi za Afrika na Nurdic unaotarajia kufanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania Novemba 8-13, ambao utashirikisha jumla ya Nchi 29 za Afrka na tano za Ulaya. Katikati ni Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jacobsen. Kushoto ni Balozi Kanali Mbuge. (Picha na Muhidin Sufiani).
**************************
 KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Faraji Mnyepe, amesema watanzania wanatakiwa kujiandaa kupokea fursa za biashara kutokana na ujio wa wageni kutoka katika mataifa mbalimbali Afrika na kutoka nchi za Nurdic. 
Hayo ameyasema leo wakati akizungunza na waandishi wa Habari juu ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje katika nchi za Afrika na Nurdic unaotarajiwa kufanyika Novemba 8 hadi 13 mwaka huu, jijini Dar es Salaam. 
Alisema mkutano huo utahusisha viongozi mbalimbali wa serikali za nchi shiriki hivyo hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara hususan wenye Hoteli nchini. 
Aidha alisema kuwa katika mkutano huo takribani Mawaziri 34 wa mambo ya nje watashiriki kutoka mataifa 5 ya Nurdic na 29 ya Afrika. 
Aliongeza kuwa pamoja na idadi hiyo pia watendaji wa serikali na wageni wengine watakaoambatana na Mawaziri hao watajumuisha idadi ya wageni kuwa zaidi ya 300.
Aidha Dk. Mnyepe, alisema Rais Dk. John Magufuli, ndiye anayetarajiwa kufungua mkutano huo na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.
Alisema pia utaratibu wa ufanyikaji wa mikutano hiyo umekuwa wa kupokelezana kwa nchi za Afrika na Nurdic kila mwaka. 
Akizungumzia ushirikiano baina ya nchi za Nurdic na Tanzania Dk. Mnyepe, alisema tangu mwaka 2013 hadi 2018 nchi hizo zimesaidia miradi mbalimbali ya nchi kwa takribani sh. bilioni 900.
Kwa upande wake Balozi wa Norway nchini Elisabeth Jacobsen, alisema mkutano huo unalenga kufanya kujadili ushirikiano wa mambo mbalimbali kwa namna ya kirafiki. 
Alisema majadiliano hayo yanalenga kutengeneza sera na mikakati ya pamoja kukuza uchumi na utoaji wa huduma muhimu baina ya mataifa shiriki. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.