Habari za Punde

UMOJA WA TAASISI ZA ACHA NA TRW WAZINDUA KAMPENI YA ELIMU YA MPIGA KURA

 Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi mbili za Action for Change 'ACHA' na The Right Way 'TRW', Michael Kyande (kulia) akikata utepe kuzindua rasmi Kampeni ya utoaji elimu ya mpiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu, nchini. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Action For Change, Martina Kabisama na Mwenyekiti wa shirika hilo, Justina Shauri. (Picha na Muhidin Sufiani).
 Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi mbili za Action for Change 'ACHA' na The Right Way 'TRW', Michael Kyande (kulia) Katibu wa TRW, Gideon Mazara, Mkurugenzi Mtendaji wa Action For Change, Martina Kabisama na Mwenyekiti wa shirika hilo, Justina Shauri, kwa pamoja wakionesha vijitabu vya elimu ya uchaguzi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya utoaji elimu ya mpiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu.Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar es Salaam, leo.
 Mratibu wa Tanea, Rhoda Kamungu, akizungumza wakati wa hafl ya uzinduzi huo.
VYOMBO vya habari vimetakiwa kuacha kuandika habari za uchochezi ambazo zitawakatisha tamaa wananchi katika chaguzi mbaimbali na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Action For Change (ACHA) Martina Kabisama kwenye uzinduzi wa kampeni ya elimu ya uchaguzi katika kusimamia uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kabisama alisema vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika jamii kwa kuelimisha au kupotosha hivyo basi vyombo hivi vinatakiwa kuwa makini kipindi hiki cha uchaguzi ili wananchi wawee kuchagua viongozi walio bora na kuweza kujenga taifa lililo bora.
Pia aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani katika maeneo yao ya ibada katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sababu viongozi wa dini wana nafasi kubwa kuaminika kwa waumini wao.
 Alifafanua asasi za Action For Change (ACHA) na The Right Way (TRW) kwa pamoja wanadhamiria kuendesha mpango wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia, na uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu, na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Action For Change, Martina Kabisama, akizungumza na waandishi wa habari. 
Alisema asasi hizi zimeungana baada ya kupata kibali cha kuendesha shughuli hizo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Septemba mwaka huu.
Alieleza kuwa  asasi hizo zinamuelekeo wa kufanya shughuli zinazofanana, hususani za uchaguzi, ambapo zina dhima ya kukuza kujiamini katika chaguzi na michakato mingine ya kikatiba kwa kuhakikisha uendeshaji bora wa michakato ya uchaguzi.
Hata hivyo alisema lengo ni kuunga mkono mabadiliko ya kiutawala kupitia elimu ya uraia, upigaji kura na uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Kwa pamoja tunataka mchakato wa uchaguzi ambao unaongozwa na wananchi unakuwa shirikishi, wenye uwazi, huru na haki,”alisema.
Alisema ACHA na TRW kwa pamoja wanatoa elimu ya uiraia, mpiga kura na uangalizi wa michakato ya chaguzi kwa kuzingatia vigezo na kanuni za Tanzania na zile za kimataifa zinazo tawala chaguzi.
“Uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ni fursa nyingine kwa watanzania kushuhudia ukuaji wa utawala wa demokrasia na ipo aja ya ushiri mpana wa wananchi wote katika mchakato huo kuanzia kipindsi cha kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi”alisema.
Pia aliongeza ACHA na TRW wana matarajia kupeleka waangalizi wilaya zote za Tanzania bara, jumla ya waangalizi wa muda mrefu 215 na watapewa jukumu juu ya ngazi ya majimbo na waangalizi wa muda mfupi 3600 watapelekwa kwenye vituo mbalimbali vya uangalizi nchi nzima.
Kwa upande wake wa Mratibu wa Tanzania Election Aliences (TANEA)Rhoda Kanungu alisema jamii inatakiwa kufahamu umuhimu wa wao kupiga kura ili kuchagua kiongozi ambaye atasimamia maendeleo ya  maeneo yao wanayoishi.
Alisema wakati huu ni sahihi wa kuwafikia wananchi na kuwapatia elimu ambayo itawasaidia kuchagua viongizi bora watakaotatua changamoto zao.
Pia alifafanua kuwa elimu ambayo wanaitoa kwa wananchi ni muhimu kufuatiliwa kwa vitendo ili iweze kutoa tija katika jamii kwa wananchi kupata viongozi wanaowataka katika mitaa yao.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa TRW Michael Kyande alisema wananchi wanatakiwa kupatiwa elimu ya uchaguzi na usimamizi wa uchaguzi ili kuweza kuwatoa hofu kipindi cha kuhesabu kura ili kuwa na imani na viongozi wao.
Aidha aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujiandisha na kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni lakini kwenye kupiga kura hawaonekani hapo hakuwezi kupatikana viongozi bora wa kuongoza serikali za mitaa.
 Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
*******************************
Kwa upande wa wananchi ambao ndiyo wapiga kura Fatuma John ambaye ni mkazi wa Kariakoo alisema jamii bado haijapatiwa elimu ya kutosha juu ya suala la upigaji kura.
Alisema jamii inatambua kuwa ukisha kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ndiyo umeshachagua kiongozi haina haja ya kujitokeza siku ya kupiga kura.
Fatuma amezitaka asasi mbalimbali za kiraia kujitahidi kutoa elimu kwa mpiga kura hasa vijijini ili wananchi waweze kuitambua haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi bora katika mitaa yao.   

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.