Habari za Punde

BREAKING NEEEEWSSS, ZAHERA 'OUT' YANGA, MKWASA 'IN'

MWENYEKITI wa Yanga, Dk. Mshindo Msolwa, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Klabu hiyo jijini Dar es Salaam, leo wakati akitangaza rasmi kuhusu Klabu hiyo kuachana na Kocha wake Mwinyi Zahera na Benchi zima la Ufundi, ambapo alimtangaza Boniface Mkwasa, kukabidhiwa timu kwa muda kabla ya mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela. 
*******************************
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera sasa ni rasmi ametimuliwa na kupewa mkono wakaheri kukinoa kikosi cha wanajangwani hao kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu ya msimu huu katika Ligi Kuu Tanzania Bara na mechi za Kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Klabu hiyo, Mwenyekiti, Mshindo Msolwa, amesema kuwa Klabu hiyo leo imeachana rasmi na Zahera ambaye msimu uliopita aliiongoza Yanga kucheza mechi 18 za Ligi Kuu Bara bila kufungwa mpaka ilipokubali kichapo kutoka kwa Wapiga Debe wa Stand United uwanja katika Uwanja wa Kambarage kwa kufungwa bao 1-0.
Aidha Msolwa amesema kuwa baada ya kumpoka nafasi hiyo Kocha Mkuu hivi sasa timu itakabidhiwa kwa muda kwa aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo na timu ya Taifa, Bonioface Mkwasa (Mkwasa Master) atakayekaimu kwa muda wa wiki mbili kabla ya kumpata Kocha Mkuu.
Mkwasa ataambatana na kikosi hicho kesho kuelekea Mtwara katika mchezo wao dhidi ya Ndanda, husu akiwa na kibarua kizito cha kusaka Watu wa Benchi la ufundi atakaoambatana nao baada ya kuvunjwa Benchi zima la Klabu hiyo hii leo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Kocha huyo Zahera anaondoka Klabuni hapo huku akiidai Yanga kiasi cha pesa ambacho hakikuwekwa wazi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.