Mkakati wowote wa kukuza uchumi unawategeme wafanyabiashara, Tukiwa kwenyekilele cha miaka 20 tangu Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni kuanzishwa ni mambo mengi tunajivunia ikiwa ni pamoja na kufankiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa urasimu na rushwa uliokithiri katika taasisi hiyo.
Heko nyingi kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kwa kubuni mfumo Madhubuti wa usajili kwa njia ya mtandao( ORS Online Registration System) Tangu mfumo huo wa ORS kuanzishwa yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa tu zaidi ya makampuni 7000 yameshasajiliwa katika mfumo huo.
Tathmini iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu imeonyesha kwa mwezi BRELA walikuwa wakisajili makampuni 60 tu lakini sasa kwa mwezi wanasajili makampuni 750 mpaka 800.
Kwa zaidi ya silimia 50 urasimu na michakato mirefu ya kupata vibali na leseni za biashara pamoja na uwekezaji umepungua kwa kiasi kikubwa. Kujisajili kwa mtandao humwezesha mfanya biashara kutambulika na hivyo kuingia kwenye mfumo wa ushindani kwenye masoko mbali mbali ndani nan je ya nchi.
No comments:
Post a Comment