Mratibu wa miradi ya ulinzi wa wanawake na watoto wa kituo cha msaada wa sheria cha wanaake na watoto WLAC, Consolata Chipote, akizungumza wakati wa Tamasha Maadhimisho ta siku ya Mtoto wa kike duniani, lililofanyika Shule ya Msingi Mbagala Kizuiani, jijini Dar es Salaam. (Picha na Nasma Mafoto)
**************************************
MRATIBU wa Miradi ambayo inahusiana na ulinzi wa wanawake na watoto katika Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), N Consolatha Chipote amesema watoto ni kundi ambalo liko kwenye hatari ya kufanyiwa ukatili, hivyo kunatakiwa kuwepo na jitihada mbali mbali za serikali na wadau wa mendeleo ya kijamii kutokomeza ukatili huo.
Chipote amesema hayo leo Oktoba 22,2020 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Toleodosia Mholo wakati wa kuadhimisha siku ya mtoto wa kike iliyofanyika katika Shule ya Msingi Annex, iliyopo Manispaa ya Temeke, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Alisema watoto wana haki ya kulindwa ili watimize ndoto zao, kwa sababu kuna baadhi ya
watoto wa kike waliyofanyiwa ukatili wa jinsia wameshindwa kuendelea na shule kutokana na mazingira yaliyowazunguka.
"Watoto ni kundi ambalo lipo kwenyehatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia, kuna takiwa kuwepo
na jitiada za haraka kutoka Serikali na kwa wadau wa maendeleo ya jamii pamoja na asasi za kitaifa kuhakikisha zinahusika moja kwa moja katika ulinzi wa mtoto," amesema Chipote
Aidha Chipote ambae ndiyo Mratibu wa Tamasha hilo, amesema mradi huo unatekelezwa katika Wilaya za Ubungo, Temeke na Kinondoni, ambapo ni mradi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa watoto.
Kwa upande wake, Afisa Elimu Msaidizi Kata ya Mbagala, Mwalimu Jemima Rengima
amesema, ukatili kwa watoto upo na hali siyo nzuri sababu watoto wanataka mitaani, kwa hiyo tunatakiwa tushirikiane na wazazi kutoa taarifa za ukatili huo.
"Mtoto anapo kueleza kwamba amepata tatizo, jaribuni kulifuatilia, kuanzia ngazi ya chini kama alipata tatizo akiwa shuleni basi waliripoti shuleni, na kama ni nyumbani basi kuna ngazi mbalimbali za kuanzia ikiwemo Serikali za Mitaa hadi kufika polisi," amesema Rengima
Amesema tangu watoto hao wapewe mafunzo kwa kushirikiana na WLAC kumekuwa na mabadiliko makubwa , kwa sababu watoto wameweza kujitambua, wamepunguza uoga na kuwapa ujasiri wa kueleza tatizo pindi tu linapompata bila ya kuona aibu.
Mratibu mwandamizi jeshi la polisi, Leah Mbunda, kutoka dawati la jinsia na watoto Kanda maalum ya Dar es Salaam, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mbagala Annex, wakipita na mabango yanayopinga ukatili kwa mtoto wa kike,
Mwanasaikolojia ya Elimu, Mhadhiri kutoka Duce, Simeon Hazole, akizungumzi kuhusu ukatili wa mwilini upande wa walimu na wazazi.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria Tamasha hilo la maadhimisho.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Kata ya Mbagala, Getruda, Nyagabona, akizungumza.****************************
Naye, Gertruda Nyagabona, Ofisa Ustawi wa Jamii, Kata ya Mbagala amesema wao ndiyo wanaohusika katika masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto, katika maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbio isemayo 'sauti yangu kwa kesho yenye sawa, ikiwa na maana kwamba tumsikilize mtoto wa kike kwa sababu, yupo kwenye kundi ambalo ni hatarishi.
Mmoja wa wazazi waliohudhuria maadhimisho hayo, Tekla Elieza amesema mtoto wa kike anakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo mara nyingi zinasababisha watoto hao kuingia kwenye mazingira hatarishi na vishawishi.
"Mfano binti anasoma umbali mrefu na kutokana na shule kuwa mbali, kwa hiyo unakuta vijana wa
bodaboda anamdanganya kwa kushawishi kumpeleka shuleni ama kurudisha nyumbani, na kwa kuwa mtoto anakuwa ameishatembea sana, anakubali kupanda bodaboda na kujikuta amepelekwa mahali pengine na kufanyiwa vitendo vya ukatili," amesema
Hata hivyo, mzazi huyo amekishukuru kituo hicho kwa msaada wa mafunzo waliyoyatoa kwa watoto wa kike na hata wazazi, kwa sababu yamekuwa msaada mkubwa kwao.
"Msaada unaotolewa na WLAC umetusaidia sana sisi kama wazazi yametufanyia wepesi wa kuweza kufuatilia watoto wetu, na tukienda kwenye vyombo husika tunasikilizwa, nina washauri wazazi ambao bado hawajajiongeza, wajiongeze ili tuweze kuwalinda watoto wetu wa kike,",amesema
Kwa upande wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Leah Mbunda kutoka Dawati la Jinsi na Watoto Kanda maalumu Dar es Salaam, amesema katika kuhakikisha ulinzi wa watoto unakuwepo, dawati linahakikisha linashughulikia makosa yanayohusiana na ukatili huo kwa haraka.
"Dar es Salaam tuna madawati zaidi ya 20 na wahudumu ni askari waliopata mafunzo waliotapakaa katika vituo vya polisi vikubwa ili kuwashughulikia wahanga wa ukatili. Tunashukuru sana WLAC kwa kutoa elimu imesaidia sana, wananchi wamepata mwamko, wamepata uelewa wa kutumia madawati yetu," amesema Mrakibu Mbunda, ameongeza kuwa, pamoja na kupokea malalamiko mengi pia wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali, ambapo kesi nyingi zinazoripotiwa hazifiki mwisho mzuri, kwa sababu zikishafika mahakamani wahanga hawaonekani.
Naye, Mwalimu wa Shule hiyo, Hassan Jeje amesema wanakishukuru kituo hicho kwa kuwapa mafunzo ya kuweza kuwalinda watoto wakiwa shuleni na nyumbani, kwa sababu hadi wazazi na
wanafunzi wamefaidika na mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment