

Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakiwa katika foleni kusubiri huduma ya kununua umeme katika Kituo cha kuuzia umeme cha Mikocheni, baada ya huduma hiyo kukosekana kutokana na hitilafu za mitandao upande wa Tanesco. Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam na mikoani kwa ujumla walilazimika kulala giza na wengine kufunga maofisi kutokana na kushindwa kununua umeme huku wengine wakinunua na kupata token ambazo hazikuweza kuingia ili kuwasha umeme huo.




No comments:
Post a Comment