Habari za Punde

RAIS SAMIA APOKEA HATI YA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA MALAWI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akijiandaa kupokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Tanzania, Andrew Posyantos Efron Zumbe, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma leo. 
Aidha Rais Samia baada ya kupokea hati hiyo alishiriki mkutano wa EAC uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Tanzania, Andrew Posyantos Efron Zumbe, mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma leo. 
Rais, Sania akizungumza kuhutubia wakati aliposhiriki katika Mkutano wa EAC uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini, Andrew Posyantos Efron Zumbe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dodoma leo. Picha na Ikulu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.