Akijibu swali Bungeni leo lililoulizwa na
Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga, lililotaka kujua maendeleo ya ujenzi wa
barabara hiyo, Naibu Waziri Kasekenya amelihakikishia Bunge kwamba ujenzi wa
barabara hiyo sehemu ya kilometa 4.5 utakamilika ifikapo mwezi Juni, mwaka huu.
Aidha, amesema Serikali inaendelea na
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Igawa – Mbeya – Tunduma ili
kupunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo muhimu kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri
Kasekenya ameliambia Bunge kuwa jukumu
la usafi wa barabara na mifereji ikiwa ni pamoja na kuzibua makalvati ni la
msimamizi wa barabara husika, hivyo kwa barabara Kuu na za Mikoa zinasimamiwa
na TANROADS na barabara za Mijini na Vijijini zinasimamiwa na TARURA.
No comments:
Post a Comment