Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA UTAFITI WA MAGONJWA NA TIBA NIMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango, akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya LAB Equipment Ltd, Hassan Razack,  wakati alipotembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye Mkutano wa 31 wa Utafiti wa Magonjwa na Tiba ulioandaliwa na NIMR katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu , (kushoto) ni Meneja wa LAB Equipment Ltd Tanzania, Rehana Mukadama. (Picha na Muhidin Sufiani)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango, akimsikiliza Meneja wa Benki ya Nmb Tawi la Bank House, Seka Urio, wakati alipotembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye Mkutano wa 31 wa Magonjwa na Tiba ulioandaliwa na NIMR katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB Tawi la Bank House, Lydia Mgweno, akifafanua jambo kwa mteja aliyetembelea katika banda lao la maonyesho wakati wa Mkutano wa 31 wa Magonjwa na Tiba ulioandaliwa na NIMR katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Uhusiano wa NMB Tawi la Bank House.Baadhi ya wadhamini wa mkutano wa 31 wa Magonjwa na Tiba wakiwa katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa 31 wa Magonjwa na Tiba ulioandaliwa na NIMR katika Ukumbi wa Juluis Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.