Habari za Punde

KOMBE LA DUNIA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI, KESHO WANANCHI KUPIGA NALO PICHA TAIFA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, (kushoto) akishuhudia Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazir, Juliano Balletti, akifunua Kombe la Dunia wakati wa hafla ya utambulisho wa ujio wa Kombe hilo nchini iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo May 31-2022.
Msema chochote akiendesha hafla hiyo.
Mwakilishi wa Cocacola Kanda ya Tanzania, Hellen Masumba, akizungumza na baadhi ya viongozi na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wa hafla ya utambulisho wa ujio wa Kombe hilo nchini iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo.
Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazir, Juliano Balletti, akizungumza na baadhi ya viongozi na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wa hafla ya utambulisho wa ujio wa Kombe hilo nchini iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, akizungumza na baadhi ya viongozi na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wa hafla ya utambulisho wa ujio wa Kombe hilo nchini iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, (katikati) na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazir, Juliano Balletti (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, (katikati) na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazir, Juliano Balletti (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi Soka nchini wakati wa hafla ya utambulisho wa ujio wa Kombe hilo nchini iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo. (Picha zote na Muhidin Sufiani)
Shughuli ikiendelea.....
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, ameipongeza Kampuni ya Coca Cola Tanzania kwa kufanikisha ziara ya Kombe Halisi la Dunia la FIFA, huku akisema hafla ya Watanzania kupiga picha na kombe hilo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, itaambatana na uoneshwaji wa Filamu ya Royal Tour.

Royal Tour ni filamu iliyorekodiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ikitangaza utalii na vivutio vilivyotapakaa Tanzania na kwamba kutokana na macho ya wadau wa soka Duniani kuelekezwa nchini kutokana na ziara hiyo, basi ni fursa kwa Watanzania kujitokeza sio tu kupiga nalo picha, bali kuona ubunifu wa Rais katika filamu hiyo.

Kombe la Dunia la FIFA limewasili nchini alfajiri ya Mei 31, kabla ya kufanyiwa utambulisho kwa wanahabari katika hafla iliyofanyika Hyatt Regency Hotel na baadaye kupelekwa Ikulu ya Dar es Salaam, lilikopokelewa na Rais Samia – Mtanzania pekee anayeruhusiwa kulishika kwa mujibu wa Sheria za FIFA.
Taji hilo limetua nchini kwa msafara unaoongozwa na Juliano Belleti, beki wa zamani klabu kadhaa Ulaya zikiwamo Villareal, Barcelona (Hispania) na Chelsea ya Uingereza, ambaye alitwaa taji hilo akiwa timu ya taifa ya Brazil katika fainali za Korea Kusini na Japan, mwaka 2002, ambako alikiri furaha kubwa kufika Tanzania.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utambulisho wa ujio, Waziri Mchengerwa awali alisema kilichofanywa na Coca Cola Tanzania – kufanikisha ujio wa taji hilo ni jambo la kupongezwa, wao kama Serikali wanaunga mkono jitihada hizo na wataitumia ziara hiyo kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Michezo ili kuharakisha ukuaji wake.

“Kesho Juni Mosi itakuwa fursa muhimu kwa Watanzania kupiga nalo picha kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Aidha, kutakuwa pia na onyesho filamu ya Royal Tour ya Rais Samia kuanzia saa 11 hadi saa 12. Kwahiyo wito wetu kwa watananazania kujitokeza kwa wingi kuja kuona matukio hayo mawili makubwa,” alisema Mchengerwa.

Tanzania inahitimisha ziara ya taji hilo kwa nchi ambazo hazijafuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, ambapo Afrika ziliteuliwa nchi nne tu, ambazo ni Ethiopia, Kenya na Afrika Kusini, na baada ya hapo, taji hilo litaanza ziara katika mataifa 32 yaliyofuzu fainali za Qatar, zikiwemo tano za Afrika.
Mkurugenzi Mkazi wa Coca Cola Kanda ya Tanzania, Hellen Masumba, alisema subira ya miaka nane kwa Watanzania kusubiri ziara ya zawadi kubwa na ya thamani zaidi duniani ya Kombe la Dunia, hatimaye kiu hiyo imekatwa kwa ziara hiyo, ambayo mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2013, na kuoneshwa dimbani CCM Kirumba, Mwanza.

“Nina furaha kuwajuza kuwa taji limetua nchini kwa jitihada za Coca Cola. Hii ni fursa kwa Watanzania kujumuika na wanamichezo hasa soka duniani kote, kwani ujio huu unafuatiliwa kote. Nichukue fursa hii kuwakaribia Benjamin Mkapa kesho ili kupiga nalo picha na kujiwekea kumbukumbu ya kudumu maishani,” alisema Hellen. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.