Habari za Punde

SPIKA TULIA AZIFAGILIA BUNGE SC, TASWA SC

Wachezaji wa vikosi vya kwanza vya timu za Bunge SC na Taswa Sc, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mtanange wao wa kirafiki uliochrzwa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. katika mchezo huo Taswa ilishinda mabao 2-0.
Kikosi cha Taswa SC.
Kikosi cha Bunge SC.
********************************
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amezipongeza timu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa SC) na Bunge SC kwa kupromoti michezo kwa kunyesha mfano kwa vitendo kwa kucheza katika mechi mbalimbali.

Spika Tulia alisema hayo wakati wa mechi maalum ya kirafiki kati ya Taswa SC na Bunge SC iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Taswa SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Alisema kuwa amevutiwa na jinsi Wabunge na waandishi wa habari na Wabunge wakionyesha vipaji vyao katika mpira wa miguu na netiboli, jambo ambalo litawafanya vijana kuiga mfano wao na kupata wachezaji nyota wa timu za Taifa.

 “Kw kweli hii imenivutia sana kwani tutawafanya vijana kuiga mfano na kuwa na wachezaji bora, nawatakia kila la kheri katika jambo hili,” alisema Tulia ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji walioichezea timu ya netiboli ya Bunge Queens iliyoifunga Taswa Queens mabao 15-13.

Mbali ya Ackson, pia Mama Salma Kikwete ni mmoja wa wachezaji nyota wa timu ya Bunge Queens ambayo inajiandaa na michuano ya Bunge la Afrika Mashariki yaliyopangwa kufanyika Juba, Sudan Kusini.

Kwa upande wake, meneja masoko wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa amefurahishwa na timu zote mbili na kampuni yao ipo tayari kusaidia timu zote katika shughuli mbalimbali za michezo na kijamii.

“M-Bet Tanzania inajisikia faraja zaidi kushirikiana na Taswa SC katika kufanikisha ziara na tukio hili, pia tupo tayari kusaidia timu ya Bunge SC katika masuala mbalimbali,” alisema Mushi.

Naye Mwenyekiti wa  Taswa SC chairman, Majuto Omary aliipongeza timu ya Bunge SC na kampuni ya M-Bet Tanzania kwa kufanikisha lengo lao la kucheza na waheshimiwa Wabunge kwa mara ya pili.

Nahodha wa timu ya Bunge SC, Cosato Chumi alisema kuwa wamepata kipimo kizuri kuelekea michuano ya Afrika Mashariki na kuipongeza Taswa SC kwa mchezo mzuri.

Wakati huo huo, Taswa SC  iliendeleza rekodi yake ya kutofungwa mwaka huu baada ya kuifunga Bunge SC mabao 2-0. Mabao ya Taswa SC yalifungwa na Waziri Idd na Zicco George.

Katika mchezo huo, Taswa SC iliongozwa na mwenyekiti wake, Majuto Omary  huku Bunge SC ikiongozwa na kepteni fundi Cosato Chumi.

Mbali ya Majuto aka Ronaldo wachezaji wengine waliongara katika mechi hiyo ni Wilbert Molandi (nahodha), Edward Mbaga, Salum Jaba, Saidi Seif, Muhidin Sufiani, Hassan Habani na kipa nyota Ismail Shaaban. Katika mchezo wa pili, Taswa SC iliifunga Utumishi Veterans mabao 3-0. Mabao ya Taswa SC yalifungwa na Waziri, Zicco na Mlanzi.

Katika netiboli,  Bunge Queens iliendelea ‘kuinyanyasa’ Taswa Queens baada ya kuichapa kwa mabao 15-13.

Kikosi cha Taswa Queens
Vikosi vya Bunge Queens na Taswa Queens wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wao wa kirafiki.
Taswa SC na Taswa Queens wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.
Taswa wakiwa na mdhamini wao kutoka kampuni ya M Bet ndani ya ukumbi wa Bunge.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.