RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan, ametoa ahadi ya kununua kila bao shilingi milioni tano kwa tii hii katika michezo yake ya Kimataifa.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
wakati akitoa salamu za Rais kwa wahariri wa Vyombo vya habari walioshiriki
katika Semina maalumu iliyoandaliwa na Shirika la Reli Tanzania jijini Dar es
Salaam leo.
Aidha Msigwa alisema kuwa Rais Samia ameamua kutoa ofa hiyo
ya kununua kila bao kwa timu hizo ili kuzihamasisha timu hizo kufanya vizuri
kwenye michuano hiyo ya kimataifa baada ya kufanya vibaya katika michezo ya o
ya awali iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Rais Samia kuonyesha kuwa anaizingatia michezo na kuumia
pindi timu za nyumbani zinapofanya vibaya katika michuano ya Kimataifa, amesema
atanunua shilingi milioni tano kwa kila bao moja litakalofungwa na Simba katika
mchezo wake dhidi ya Raja Casablanca ya nchini Moroco ukiwa ni mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa
kwa simba utakao chezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi wiki hii,
Hivyo hivuo kwa Yanga itakayocheza mchezo wake wa pili wa
Ligi ya Shirikisho dhidi ya T-P Mazembe kutoka Kongo mchezo utakaochezwa
Jumapili wiki hii baada ya timu zote kupoteza michezo ya awali ya ugenini.
No comments:
Post a Comment