Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewaongoza wakaazi wa Jiji la Dar es salaam na Watanzania kwa ujumla kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) ambayo ni mashindano yenye hadhi kubwa zaidi katika kandanda barani Ulaya.
Mhe. Chana ameungana na wakaazi hao ambao walifurika katika viunga vya Mlimani City jijini hapo Juni 10, 2023 kushuhudia fainali hiyo kati ya timu ya Manchester City ya nchini Uingereza na Inter Milan ya nchini Italia ambapo Manchester City imeibuka Mabingwa kwa ushindi wa Goli 1-0.
Dkt. Chana ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Saidi Yakubu, amewapongeza Heineken Tanzania kwa ubunifu wao wa kuwaletea furaha watanzania kwa kuonesha mchezo huo kwa miaka miwili mfululizo ambapo mwaka 2022 fainali hiyo ilioneshwa eneo la daraja la Tanzanite.
No comments:
Post a Comment