Habari za Punde

Chibulunje, augua ghafla Bungeni, Tukio kamili

Naibu wa Miundombinu, Ezekiel Chibulunje, akianza kusoma jibu la swali la, Mbunge wa Kalenga, Steven Galinoma, swali lililoonekana kuwa gumu kama jiwe kiasi cha kumfanya chibulunje kuugua na kupokewa na Waziri wake kumalizia kujibu naye akakimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. hata hivyo hali yake iliendelea vyema na kuruhusiwa siku hiyo jioni. Picha na (SPM)
Chibulunje, akianza kubanwa na pumzi, hapa akishika kifua kuashirika kubanwa mapigo ya moyo kutokwenda sawa. Picha na (SPM)

Chibulunje asaidiwa kuondoka kwenye sehemu maalum ya kuzungumzia Mawaziri, na mmoja wa Wabunge, baada ya Naibu Spik, Anna Makinda, kutoa kauli kuwa asaidiwe.


Chibulunje, akisaidiwa.................



Waziri wa Chakula na Ushirika, Stephen Wasira (kushoto) na Waziri wa Elimu, Prof. Jumanne maghembe wakifika kutoa msaada, huku wabunge wengine wakionyeha kushikwa na mshangao.




Kila Mmoja alijitahidi kujaribu kutoa msaada wa huduma ya kwanza kwa Chibulunje, anaonekana Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, David Mwakyusa, Magembe, na Maua Daftari, wote wakijongea kutoa msaada.





Chibulunje, akisaidiwa kukaa kwenye nafasi yake kabla ya kuinuliwa kuelekea Hospitali ya mkoa dodoma kwa matibabu.






Wabunge na maofisa usalama, wakimsindikiza Chibulunje, kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kuelekea Hospitali.







Wabunge wakibaki na mshangao???????????????, huku jopo la madaktari likimsindikiza Chibulunje......








No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.