Habari za Punde

Ubize wa Simu za Mkononi

Kaka pita huko basi tusigongane, kwani we huoni?........ Wakati mwingine unaweza kuonekana kama tofauti na wenzako na hasa pale unapokuwa bize na simu yako ya mkononi, hata unaposemeshwa unaweza usisikie kutokana na kwamba akili zako zote kwa muda huo zimehamia katika simu yako, kama jamaa hawa wanavyoonekana kila mmoja kwa wakati wake akitumia simu bila kujua kuwa wanaoweza kuonekana kituko mbele ya watu kutokana na ubize wao unaofanyika kwa wakati mmoja na sehemu moja. Picha na (SPM)
Hakia......Buku langu utanipa la sivyo nakupasua...... Vijana ambao hawakuweza kufahamika majina yao mapema, wanaojitafutia riziki ya kila siku kwa kuosha magari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma wakipimana ubavu baada ya kudhurumiana BUKU, ambalo mmoja wao alilipwa na mteja wao na kudhurumu mwenzake. Picha na (SPM)

Mtaji wa masikini ni 'Nguvu zake Mwenyewe'....... Mkazi wa Manispaa ya Dodoma akikokota mkokoteni uliosheheni matenga matupu. Matenga hayo hutumika zaidi kusafirishia nyanya na matunda mengine kutoka mikoa ya jirani. Picha na (SPM)


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.