Mrembo Gisela tarimo, akiwa katika pozi pembeni mwa Bwawa la kuogelea.
Habari Njema kwa Watanzania
GISELA Tarimo (20) mwakilishi pekee wa Tanzania, ameibuka mshindi wa tatu wa Tuzo ya Miss Personality, (mrembo mwenye mvuto) katika Mashindano ya Miss Tourism Queen International ambayo yamefanyika Agosti 28 mwaka huu,huko Zhenghou nchini China, na kushirikisha jumla ya warembo 120 kutoka nchi mbalimbali Duniani.
Gisela ambaye aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi wa nane, alifanikiwa kushinda tuzo ya Miss Personality nafasi ya tatu 2009 na kupewa cheti.
Mbali na uhalisi wa rangi na nywele zake pia nguo za mrembo huyu zilitoka kwa wabunifu mbalimbali wa hapa nchini wakiwamo Maua Mazuri, Mama Ailinda Sawe wa Africa Sana na Fatma Amour (Fatma style na mbunifu chipkizi toka mkoani Morogoro Diana ambaye alimbunia vazi la Taifa (National Costume).Katika kinyanganyiro hicho Gisela ndio alikuwa mshindi wa tatu kushinda tuzo hiyo.
Ukiondoa Miss Personality pia kulikuwa na tuzo nyingine kama Miss Photogenic, National costume, Friendship, Charity, Elegant, Miss Bikini, Miss Charm, Miss Talent na Miss Disco,Katika kinyanganyiro hicho Miss Russia aliibuka mshindi wa kwanza, mshindi wa pili alitoka nchini Brazil na mshindi wa tatu alitoka nchini Guinea.
Na washindi wengine walioingia katika tano bora ni pamoja na China na French Polynesia. Mrembo Gisela amewasili nchini jana mchana na ndege ya Qatar air kutoka nchini China ambako alikwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Miss Tourism Queen International.
No comments:
Post a Comment