Habari za Punde

Mpakanjia afariki Dunia, kuzikwa kesho

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MPAKANJIA MAHALA PEMA PEPONI, AMINA!.... CHA YA MEDY MPAKANJIA ENZI ZA UHAI WAKE AKIWA KATIKA POZI

IKIWA ni siku moja tu baada ya kuchukua uamuzi wa busara, kuchukua jiko (kuoa) mwanamke wake kipenzi ajulikanae kwa jina la Zaitun, katika Mtaa wa Tosheka Magomeni, tangu alipoondokewa na mkewe kipenzi Amina Chifupa, mfanyabishara hyuo amefariki Dunuia leo mchana katika Hospitali ya Lugalo, ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Habari zilizotufikia kutoka kwa baadhi ya wanandugu wa karibu wa mfanyabishara huyo maarufu, aliyekuwa na makazi yake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, zimedai kuwa Meddy alianza kusumbuliwa na maumivu makali siku mbili kabla ya umauti wake, ambapo alipelekwa kwenye Hospitali binafsi ya Dk. Massawe iliyopo Temeke na kugundulikwa kuwa alikuwa na homa ya matumbo (typhoid).
Baada ya vipimo hivyo, Dactari wake alidai kuwa marehemu alibahatika kuwa na nguvu za kutosha hadi muda kuo kutokana na ugonjwa huo kuwa tayari ulishaenea mwilini kote.
Kwa mujibu wa watu alioongozana nao hospitalini hapo, baada ya muda Meddy, alianza kupoteza nguvu na nduguze walichukua jukumu la kumuhamishia katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo, ambako ulimkuta umauti mida ya saa saba mchana.
Meddy aliondokewa na mkewe kipenzi, Amina Chifupa mwaka 2007 na kufuatia kifo hicho Meddy ameacha watoto watau aliozaa na mama zao tofauti, Abdulkarim, Abdulrahim na Abdulrahaman.
Aidha mazishi ya mfanyabiashara huyo yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini
Dar es salaam, leo mchana.
SPM:- inawapa pole ndugu jamaa na marafiki wa karibu na familia ya Mpakanjia, na wale wote walioguswa kwa na namna moja ama nyingine na msiba huo. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Mpakanjia, Amein.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.