Habari za Punde

KAMANDA KOVA ATUMIA HELKOPTA KUAPIGA DORIA DAR

Nyie mnajua kuimba wimbo wa Taifa nyie!?..haya imbeni, hii ndo maanda ya uchaguziMkuu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, akisalimiana na wananchi wa Mtaa wa jangwani, baada ya kutua na helkopta ya Polisi kwenye viwanja hivyo, wakati alipokuwa akizunguka kwenye anga ya jijini la Dar es Salaam, kuhakiki usalama katika Vituo vya kupigia kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini kote leo. Picha na (SPM)

Inaonekana hali ni shwari kote Dar mbona hakuana vurugu wananchi wame....teh teh teh teh...Wananchi wa Mtaa wa Jangwani Dar es Salaam, wakiishangilia Helkopta ya Polisi iliyokuwa ikiondoka kwenye Viwanja vya Jangwani na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, aliyekuwa akizunguka katika anga ya jijini kukagua usalama wakati wa zoezi la kupiga kura leo.

Hakuna hata rimtu rimoja rifanye furugu turitie humu tukarifundishe adabu.....Magari ya Polisi la kumwaga maji ya kuwasha (nyuma) na la kubebea watuhumiwa, yakipita katika mitaa ya Tandale, Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhakiki usalama wakati wananchi wakiendelea na zoezi la kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa nchini kote leo. Picha na (SPM)

Ehee aroo nakupata, hapo ni ...umesema kote shwari sio haya endereeni na ridoria.....Mkuu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, akitumia redio ya upepo kuwapata mawasiliano na askari wake kuhakiki zoezi la kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za Mitaa linakwenda sawa.

Naona mamtu yameogopa yaone yameturia tuuu, Dereva pinda huku twende pande za Kawe...Helkopta ya Polisi ikiwa hewani ikiranda katika anga ya jiji la Dar, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova kukakua maeneo yenye vurugu leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.