Taasisi ya Mikopo ya Easy Finance, imetoa mchango wa Shilingi Milioni 12.5 kukisaidia Chama cha Soka cha Zanzibar, ZFA, kufanikisha mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kurindima huko Zanzibar hivi karibuni.
Hafla fupi ya makabidhiano, imefanyika jana mjini Zanzibar ambapo Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ, Juma Shamhuna alipokea hundi hiyo kwa niaba ya ZFA, na kuipongeza Easy Finance kufafadhili Kombe la Mapinduzi, pia alitoa wito kwa wafadhili wengi zaidi kuzidi kujitokeza kufadhili michezo visiwani humo.
Akikabidhi hundi hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Easy Finance, Isaack Kasanga, amesema Easy Finance, imetoa mchango huo kwa ZFA, ili kuonyesha inathamini juhudi za ZFA, kuboresha mchezo wa soka Visiwani Zanzibar.
Bwana Kasanga amesema pia mchango huo ni namna ya kurudisha fadhila kwa jamii wa Wazanzibari kwa jinsi wanavyoiunga mkono taasisi ya Easy Finance ambayo inalo tawi wisiwani Zanzibar.
Hii ni mara ya pili kwa Easy Finance kufadhili michezo Zanzibar ambapo mara ya kwanza, ilitoa ufadhili wa shilling milioni 5 katikati ya mwaka huu. Easy Finance, ni taasisi ya mikopo inayotoa mikopo ndani ya muda mfupi na masharti rahisi, ina makao makuu mjini Dar es Salaam na matawi Zanzibar , Mwanza na Mbeya litafunguliwa hivi karibuni.

No comments:
Post a Comment