Habari za Punde

ZAIN YAZINDUA MAONYESHO YA SARAKASI YANAYOANZA ARUSHA KESHO

Wasanii wa kundi la sarakasi la Mama Africa, wakionyesha umahiri wao.
Meneja masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu kampuni hiyo kudhamini maonyesho ya Sarakasi 'Zain Mama Afrika Sarakasi' yatakayofanyika kwenye Viwanja vya AICC, mjini Arusha kesho na kuendelea kwa wiki nne. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano Mallya uzinduzi huo ulifanyika leo mchana kwenye Ofisi za Zain kijitonyama Dar es Salaam. Zain ni kampuni ya kwanza kuleta maonyesho haya ya sarakasi nchini Tanzania. Picha na (SPM), Picha ya juu ni wanasarakasi hao wakionyesha umahiri wao.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.