Habari za Punde

MATUKIO YA BURUDANI YA WIKI JIJINI DAR, JK NA WAREMBO

Karibubuni sana warembo......
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea zawadi ya picha ya kuchorwa kutoka kwa Miss Kenya, Tabitha Mumbi (kulia) na Miss Tanzania, Julieth William, wakati warembo wa Miss East Africa 2009, walipomtembelea Ikulu Dar es Salaam juzi usiku na kushiriki naye chakula cha usiku. Shindano la kumsaka Miss East Africa 2009, lililofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Picha zote na (SPM)
Rais Jakaya Kikwete (katikati) Mama Salma Kikwete na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, wakifurahia jambo wakati wa hafla ya chakula cha usiku na warembo wa East Africa Ikulu Dar es Salaam juzi usiku

Rais Jakaya Kikwete (katikati), Mama Salma Kikwete (watatu kulia), Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika (watatu kushoto) na baadhi ya viongozi wa Kamati ya shindano hilo la miss East Africa, wakiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Miss East Africa, wakati walipoalikwa Ikulu Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete, akiagana na warembo wa Est Africa 2009, mara baada ya kumaliza hafla ya chakula cha usiku.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Warembo wanaotarajia kushiriki shindano la kumsaka Miss East Africa, wakati walipoalikwa chakula cha jioni Ikulu Dar es Salaa.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.