Habari za Punde

YANGA USO KWA USO NA MNYAMA NUSU FAINALI TUSKER

"Mie ndo Tegete bwana na bado hili ndo goli la tano katika michuano hii mtanikoma babake."Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akiusindikiza mpira wavuni kuandika bao la pili dhidi ya Tusker ya Kenya wakati wa mchezo wa hatua ya Robo fainali, mchezo uliochezwa mwisho wa wiki hii kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Yanga ilishinda 3-1. Kwa hatua hiyo Yanga itavaana na Mnyama Simba katika Hatua ya nusu Fainali mchezo utakaochezwa Alhamisi kwenye Uwanja mpya wa Taifa. Picha Zote na (SPM)

"Na bado mtaona mengi ya Canada me ndo 'Canavaro' babake"
Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' (kulia), akipongezwa na Kigi Makasi mara baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Tusker ya Kenya.

Canavaro, akiweka mpira kimiani na kumuacha kipa wa Tuske akihangaika kuutoa mpira kwenye chaki.

Canavaro, akiruka juu kupiga kichwa na kuiandikia timu yake bao la kwanza dhidi ya Tusker.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Godfrey Boni (kushoto) akichuana kuwani mpira na beki wa Tusker.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.