
Ephraem Mafuru (katikati) na Rwejuna wakipakia mbuzi kwenye gari tayari kuelekea kwenye Vituo vya kulelea Watoto Yatima kwa ajili ya kukabidhi misaada ambayo hutolewa na Kampuni ya Simu za mkononi Vodacom kupitia Kitengo cha Vodacom Faundation kila mwaka. Picha Zote na (SPM)

Msanii wa miondoko ya muziki wa kizazi Kipya, Mzungu Kichaa, akishambulia jukwaa wakati wa hafla ya kuwakabidhi misaada watoto wanaoishi kwenye Vituo hivyo vya jijini Dar es salaam inayotambulika kama, Share and Care, iliyofanyika jijini mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Dietlof Mare, akisoma hotuba yake wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Dietlof Mare (katikati) Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Faundation, Mwamvita Makamba (wapili kushoto) wakijumuika kuimba kwa pamoja wimbo wa We are the World, wakati wa hafl ahiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacoma wakicheza na baadhi ya watoto Yatima walohudhulia hafla hiyo kwa niaba ya wenzao kwenye viwanja vya New World Cinema.

Kundi la Sanaa la Wanne Star likishambulia jukwaa, kutoa burudani.

Ronald Ocen Baare wa Kampuni ya Vodacom (kulia) akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali Ofisa Ustawi Msaidizi wa Kituo cha Yatima cha Kusani, Jack Omar, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipotembelea Kituo hicho na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 3.3 jmwishoni mwa wiki.

Rukia Mtingwa (kulia) na wenzake hawakuwa nyuma katika suala zima la makulaji wakati wa hafla hiyo hapa wakijisevia.

Kundi la Wane Star likishambulia jukwaa, hii si miti bali ni binadam.

Wasanii wa kundi la Wane Star wakicheza pamoja na watoto waliohudhulia hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment