Habari za Punde

MEDIA DAY YAFANA WAANDISHI WACHIZIKA KINOMA

Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo (katikati) akiwaongoza wanamuziki wake kutoa burudani kwenye Tamasha la Siku ya Waandishi wa Habari (Media Day) lililofanyika kwenye Ufukwe wa Msasani Club mwishoni mwa wiki.

Kumbe na waandishi nao huwa wanachizika namna hii??????????, ebwana hapa ni hapo sasa hapo, hapo sasa hapo hakuna aliyekaa si unaona hata wazee wa vitambi wameinuka na kuselebuka.
Hakai mtu hapa ni siku yetuuuuuuuuuuuuuu, ndivyo walionekana kusema waandishi hawa.

Minengua si kina Aisha Madinda Pekee, hata kina dada zetu waandishi nao wanaweza hawa ni Sara Gazeti la Mtanzania (kushoto) na Khadija wa Tanzania daiam wakisakata sebene.

Wengine si kutangaza au kuwahoji kina E'too tu bali hata kucheza wanaweza, huyu ni mtangazaji wa Redio Tanzani na Televisheni ya Taifa, Evance, akiselebuka.

Huyu ni Alima Mlacha (kulia) wa gaeziti la Habari Leo, akilisakata na dereva wake.

Waandishi wakiskata sebene.

Sehemu kama hizi hapakosi vituko, huyu si mwingine ni Iche Mang'enya akicheza jukwaani na kuchekesha walonuna
Wacha nijimwage mie na misebene yangu jamani, huyu ni Khadija Khalili, akisakata sebene kwa staili yake, Wakigoma nao wamoooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

Hapo sasa hapo, hapo sasa hapoooooooooooo................................

Sijui huyu jamaa ninaemjua mimi alikuwa tayari ameshapombeka ama lah!, oseph Kapinga Mhariri wa Michezo Gazeti la Alasiri, aking'ang'ania kiuno babake, lakini ni sebene tu jamani ndo furaha hiyo
Kapinga katika pozi jingine twende sasaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Kapinga Kapinga ohooooo!

Yasha kuwa hayo Kapinga shauliyakooooooooooooooooooooo!

Hawa Mashostito nao walikuwepo katika kunongesha Tamasha si wengine ni Mwani Nyangasa (kulia) na Usu Emma, wakipiga stori kwa raha zao babake.

Sufianimafoto nae hakuwa tofauti na wenzake kwani alijichanganya na kupiga soka, Hapa anaonekana akimzungusha ama kumpa mwili jamaa wa Gazeti la Changa Moto, wakati wa mpambano wao.

Kinadada wa Business Time na Guardian, wakichuana katika mchezo wa Netiboli.

Nyabo, akiruka kupiga mpira wakati wa mcezo wa Voliboli.

Eti na Mdhungu nae alikuwepo, lakini aliumia baada ya kuangukiwa na goli na kumpasua sehemu ya kicha, hapa akipatiwa huduma ya kwanza.

Huyu ni Mkurugenzi wa Redio One Deo Rweyunga, kushoto) akimkabidhi kikombe mshindi wa Riadha upande wa Wanaume, Hatim Naheka wa Dar Leo.

Jamaa wakimshangaa mbadala ya kumsaidia, hapa akihangaika kufunga jeraha ili kupunguza damu.
Katika Tamasha hilo si michezo pekee iliyokuwa ikifagiliwa bali hata wapenzi pia, Jamaa huyu yeye alishiriki mchezo wa kukaa na mpenzi wake tuuuuuuuuuuu.

Waandishi wakichuana katika mchezo wa Voliboli.

Waandishi wa Magazeti ya Business Time, wakishangili kwa pamoja mara baada ya kukabidhiwa vikombe katika michezo yote walioshinda.























No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.