
Mashabiki wa Yanga, wakisebeneka kwa furaha, baada ya mchezo.

Mashabiki wa Yanga wao ilikuwa ni furaha iliyopitiliza, hapa wakishangili wakati mcheo ukiendelea, baada ya Jerry Tegete, kuipatia timu yake ya Yanga bao la kwanza kunako dakika ya 74 ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Sufianimafoto inawapa pole wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine Sikukuu hii ya X- Mas kwao imeinggia doa kwa maana ya kwamba furaha yao haijatimia, na pia inawapa pongezi wale wanaoendelea na furaha kutoka Uwanja wa Taifa jana hadi mitaani hii leo. Picha Zote na (SPM)

Kocha wa Simba hakuwa nyuma katika kuwapa moyo wachezaji wake kwa kuwapa maelekezo ya hapa na pale ili kuweza kurudi katika duru la pili la dakika 30 za nyongeza, baada ya kumalizika kwa dakika 90 na kutoka sale ya 1-1.

Baadhi ya Viojngozi wa Yanga na wachezaji wakishangilia mara baada ya mchezo huo wakiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Kocha wa Yanga, Kostadin Papic, akizongwa na mashabiki wa Yanga wakati wakishangili ushindi baada ya mchezo huo kumalizika.
Mnasikia jitahidini yule, wanaemwita O nini sijui asipite wala kupiga shuti Ok?....na mkifika katikati wachanganyeni kwa pasi fupi fupi sawa!

Kocha wa Yanga, Kostadin Papic (kushoto) akiwapa maelekezo jinsi ya kuwakabili wapinzani wao Simba, katika dakika 30 za nyongeza.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Jerry Tegete (katikati).

Hii ndiyo chengwa atakayoikumbuka daima Kelvin Yondan wa Simba, iliyomsababishia ugonjwa baada ya kutokwa na Mrisho Ngasa na kumimina krosi iliyozaa bao la pili, lililofungwa na Shamte Ally.

Papic, akishangilia kwa staili ya kufanya mazoezi uwanjani, kama anakimbia riadha vileeeeeeeee!

Kocha wa Simba, Patrick Phiri, akionekama kama analia, macho yamemuiva baada ya mchezo kumalizika

Beki wa Simba, George Owino (kulia) akimdhibiti, Mrisho Ngassa, wa Yanga, wakati wa mchezo huo.
Hapana Refa siyo goli mwangalie mshika kibendera alishainua juu, ni off side huyo....

Kipa wa Simba akionekana kulalamika kukataa goli lililofungwa na Mrisho Ngassa, hapa anaonekana akimuonyesha mwamuzi amuangalie mshika kibendera, aliyekuwa tayari ameshainua juu.

Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' akijilaumu baada ya kukosa goli kwa kupiga kichwa krosi iliyopigwa na Kigi Makassy.

Kipa wa yanga, Yaw Berko (katikati) akichuana na Mgosi. Baada ya action hii kipa huyo aliumia na kutolewa nje.
Hii si Kung Fu bali ni Soka

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Abdi Kassim 'Babi' akianguka baada ya kuchezewa vibaya na Jerry Santo wa Simba.
Anakwenda pale la la la la.....anakosa paleeeeeeeeee

Watangazaji wa Star Tv, James Range (kulia) na Neema Naniliu, wakitangaza mtanange huo.

Mrisho Ngassa wa Yanga (kushoto) akimtoka beki wa Simba, Juma Jabu.

Beki wa Simba, Salum Kanoni, (kulia) akiondosha moja ya hatari mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete.
No comments:
Post a Comment