Mwenyekiti wa Chama cha (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (kushoto) akiwa na Mchungaji Willbert Ngowi, wakitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam mara baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumkashifu Rais Kikwete kwa kumuita Gaidi, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8 mwaka huu itakaposikilizwa kwa mara ya kwanza.
Haya ni baadhi ya manjonjo, mapozi na vituko vya Mchungaji Mtikila wakati akitoka nje ya kwenye Mahakama hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (kulia) akiagana na Askari Magereza mara baada ya kuachiwa kwa dhamana wakati akitoka ndani ya chumba cha Mahabusu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana. Keshi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8 mwaka huu itakaposikilizwa kwa mara ya kwanza. Kushoto ni mkewe, Georgia Mtikila.
Mchungaji Willbert Ngowi (mbele) akibeba mizigo ya Bosi wake Mchungaji Mtikila, wakati akitoka kwenye Chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam jana mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Mchungaji Mtikila (kulia) akishunga ngazi kutoka Mahakamani hapo leo asubuhi, nyuma yake ni mdhamini wake wa Chama cha (DP), Anna Mkumbwa.
No comments:
Post a Comment