Habari za Punde

*NAIBU WAZIRI WA MICHEZO, KUWAPA TANO WAENDESHA PIKIPIKI DAR

Mtaalam wa kuendesha na kucheza na baiskeli ya Taili moja, Dickson Ngole, akionyesha umahiri wake wa kuchezea baiskeli hiyo wakati wa mazoezi ya waendesha Pikipiki na Baiskeli yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Bendera, anatarajia kuwatembelea waendesha pikipiki kwenye Viwanja vya hivyo mwishoni mwa Wiki hii ili kujua matatizo yanayowakabiri ikiwa ni pamoja na kufanya jitihada za kuuendeleza mchezo huo unaoonekana kupoteza mwelekeo kwa kusahaulika zaidi na Serikali na wadau wa michezo.

Mwendesha Pikipiki, Rashid Kiparacha, akiruka tuta wakati alipokuwa kwenye mazoezi katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Dar es Salaam hivi karibuni.

Mwendesha Pikipiki, Kitimutimu Aidan, akionyesha umahiri wake wa kucheza na pikipiki wakati ikiwa kwenye mwendo mkali wakati alipokuwa kwenye mazoezi katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Dar es Salaam hivi karibuni.
Waendesha Pikipiki Dotto Juma (kmbele) na Kitimutimu Aidan, wakiruka tuta kwa pamoja wakati walipokuwa kwenye mazoezi yao kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Dar es Salaam hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.