Habari za Punde

*NEW HABARI WASHEREHEKA KUMALIZA MWAKA NA KUUANZA 2010

Ni Sebene tuuuu kwenda mbele, ilikuwa ni furaha ya kumaliza mwaka na kuuanza mwaka mpya bila matatizo katika majukumu ya kazi.
Herieth Mandari (kushoto) na Rachel Mwiligwa, wakila pozi katika meza yao isiyosheheni kilaji eti hawatumii kilaji sijui ni kweli???????? ama zuga tuuuuuu!...., wakati wa Sherehe ya wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd, ya kumaliza mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka 2010, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Ocean View Giraffe Mbezi Beach Dar es Salaam jana usiku.

Hawa ni wataala wa IT ndani ya New habari wakila gambeeeeeee.

Mwandishi wa habari za Michezo wa gazeti la The African, Mwani Nyangassa (kushoto) akirekebisha mambo mezani kwake ili kuweza utaratibu wa kuendeleza gambeeee na wenzake katika meza hiyo.
Mhariri wa Habari wa gazeti la Rai, Mayege S. Mayage (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa sherehe hiyo.

Weweeeeee, aaaaiiiii, kama Michael Jackson vileeeeeeeeee, hawaniwezi sina mpinzani hapaaaaa!
Msanifu Kurasa wa gazeti la Bingwa, Susan Senga, akionyesha umahiri wake wa kucheza miondoko ya Funk, wakati was herehe hiyo.

New Habari haijambo kwa warembo, Kushoto ni Sia na Naniliu kasema nisitaje jina lake, wakiwakilisha katika sherehe hiyo.

Baadhi ya Wafanyakazi wa New Habari 2006 Ltd, wakigonganiasha glasi wakati wa sherehe yao ya kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2010, iliyofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View, iliyopo Mbezi beach Dar es Salaam.
Hii ni Miondoko ya Mduara, Vimwana wa New Habari wakisebeneka na Mduara katika Sherehe Hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.