Habari za Punde

*PSPF KUKOPESHA NYUMBA, YATOA MSAADA WA SHUKA OCEAN RD HOSPITAL DARukopesha nyumba

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma, PSPF, Bibi Hawa Mmanga (katikati) na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bw. Ali Kiwenge wakiwa ameshika moja ya mashuka 300 ambayo PSPF imekabidhi kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Rd, Kulia ni, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUGHE. Mashuka hayo 250 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 4 ni sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.


Na Mwandishi Wetu

Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma, PSPF, unaendeshwa kwa mafanikio makubwa, yanayopelekea kuzidi kutoa mafao bora kwa wanachama wake, ikiwemo mikopo ya kujenga au kununua nyumba kwa wastaafu waliobakisha miaka 5 kabla ya kustaafu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii ya Watanzania.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga, mashuka 550 na foronya zake yenye thamani ya Shilingi Milioni 8 kwa Hospitali za Temeke na Taasisi ya Saratani ya Ocean Rd zote za jijini Dar es Salaan, kama sehemu ya huduma za PSPF kwa jamii ya Watanzania, kufuatia mfuko huo kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 11 iliyopita.

Bibi Mmanga amesema, mafanikio hayo makubwa ya PSPF, yanatokana na juhudi zinazofanywa na uongozi na wafanyakazi kwa ujumla, ambapo mfuko huo unapata faida kubwa katika vitegauchumi vyake mbalimbali, vinavyo zalisha faida kubwa hivyo kuboresha mafao ya wanachama wake na ziada kutumika kwenye kutoa huduma za jamii vikiwemo vifaa na vifaa tiba kwa mahospitali.

Naye Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la PSPF , Bw. Ali Kiwenge, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUGHE, amesema, zaidi ya kutoa mafao ya uzeeni, mfuko huo wa PSPF unatoa mafao ya ulemavu, mafao ya warithi, mafao ya wategemezi na msaada wa mazishi. Sambamba na mafao hayo , mfuko huo pia unatoa mikopo ya ujenzi au ununuzi wa nyumba kwa wanachama wake waliobakiza miaka 5 kabla ya kustaafu.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Temeke, Dr. Aisha Mahita, aliushukuru mfuko huo kwa msaada wake wa shuka hizo 300 ambao amesema utasaidia sana kupunguza nakisi ya mahitaji halisi. Hata hivyo, alisema hospitali hiyo bado inakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawa, vitanda, majengo na vifaa tiba kufuatia ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji kuhudumiwa na hospitali hiyo, hivyo ametoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa PSPF.

Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Rd, Bi. Mary Haule, amesema hospitali hiyo ambayo ndio pekee ya rufaa za ugonjwa wa saratani hapa nchini, inakabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa, hali inayopelekea kuongezeka kwa mahitaji ya miundo mbinu, wafanyakazi, madawa na vifaa tiba ili kukidhi mahitaji halisi.

Mfuko huo wa PSPF ulioanzishwa mwaka 1999, unaendelea na kampeni yake maalum kuzisaidia hospitali mbalimbali nchi nzima kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, mafanikio ya miaka 10 tangu kuwepo kwake. Kesho PSPF itatoa msaada hospitali ya Temeke na keshokutwa, Hospitali ya Ilala.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.