Pole sana Kaka na samahani kwa kukutesa we tulia hivyo hivyooooo!
Mrisho Ngassa (katikati) na Idd Mbaga wa Yanga wakishangia bao la pili lililofungwa na Mrisho Ngassa.

Ivo Mapunda wa African Lyon, akiruka kuokoa moja ya michomo iliyoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo huo.
Goli lenyeutata…..

Beki wa Timu ya African Lyon, Aziz Issa, akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Jerry Tegete wa Yanga na kuandika bao la kwanza, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mzunguko wa pili uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Bao hilo lilizua mtafaruku, gumzo na ubishi baina ya mashabiki huku kila mmoja akisema vyake kulingana na jinsi macho yake yalivyokuwa na upeo wa mwisho kuona heka heka ya goli hilo.
Ufupi nao wakati mwingine noma….hapa hupiti kirahisi weweee hebu cheki nilivyokuzidi urefu!
Beki wa Africa Lyon Zubeir Ubwa (kulia) akimdhibiti, Mrisho Ngassa.
Hii Si Kung Fu la hasha ni Soka….
Beki wa Africana Lyon, Zubeir Ubwa (kulia) akiinua daluga kupiga mpira mbele ya beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa.

Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (katikati) akimdhibiti beki wa African Lyon ili kumiliki mpia wakati wa mchezo huo.

Athuman Idd (Chuji) akimdhibiti Yusuf Soka, wakati wamchezo huo.

Mabeki wa Yanga Nadir Haroub na Athuman Idd, wakiruka kwa pamoja kumdhibiti mshambuliaji wa African Lyon, Yusuf Soka.

Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (katikati) akichuana kuwania mpira na beki wa African Lyon, Abdul Musenga, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mzunguko wa pili ulioanza jana kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0. Picha Zote na (SPM)
No comments:
Post a Comment