Habari za Punde

*SHINDANO LA 'FYATUA CHOO NA USHINDE' LAFIKIA TAMATI

Kiongozi na Mkurugenzi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto (katikati) akiimba na wanamuziki wa bendi yake, Nurueli Mbowe (kulia) na Ismail Kipillah (wapili kushoto), wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la Fyatua Choo na ushinde lililofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Picha Zote na (SPM)
Marry Lucas (kulia), Nurueli Mbowe (katikati) na Ismail Kipillah, wakiimba katika hafla hiyo.

Wasanii wa Maigizo wa Kundi la Mjomba Band, 'Smaku' (kulia) na Asha Salim, wakiigiza katika hafla hiyo.
Smaku na Asha, wakitoa burudani ya maigizo kwa mbwembwe....."Si nilikwambia uchimbe Choo? sasa unaona majirani wametufukuza kujisaidi kwenye vyoo vyao.

Smaku na Asha kazini........

Vumilia Omary 'Kinailoni' (kushoto), Smaku (katikati) na Asha wakiigiza.......

VYOO VINGINE NNI NOMA JAMANI HEBU CHEKI HIVI ........................
Hizi ni baadhi ya picha za vyoo vilivyoingia kwenye mashindano ya kutuma picha za Vyoo tofauti tofauti kila kimoja kikiwa na sura yake..., uzuru wake na ubaya wake......



Hizi ni zawadi zilizoandaliwa kwa washindi waliotuma picha hizo.......


Mmoja wa waratibu akihakiki zawad hizo........

Baadhi ya wakazi wa jiji Dar es Salaam, waliojitokeza kwenye hafla hiyo, wakiangalia picha za vyoo hivyo zilizokuwa zimewekwa uwanjani hapo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa. David Mwakyusa (wapili kulia) Naibu Waziri, Dk. Aisha Kigoda (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Brandina Nyoni (kushoto) wakionyeshwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Afya na Mazingira wa Wizara ya Afya, (MOHSW), baadhi ya picha za vyoo vilivyoshindanishwa katika shindano la Fyatua Choo na Ushinde, lililofikia tamati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Brandina Nyoni (kushoto), akibadilishana Mkataba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng. Christopher Sayi, baada ya kutiliana saini Mkataba huo wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za Afya na usafi wa mazingira. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam janwakati wa hitimisho la shindano la Fyatua Choo na Ushinde, lililofikia Tamati.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa. David Mwakyusa (wapili kulia) Naibu Waziri, Dk. Aisha Kigoda (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Brandina Nyoni (kushoto) wakionyeshwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Afya na Mazingira wa Wizara ya Afya, (MOHSW), baadhi ya picha za vyoo vilivyoshindanishwa katika shindano la Fyatua Choo na Ushinde, lililofikia tamati.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.