Habari za Punde

*MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA NDANI YA JIJI LA DAR

Meneja wa Nembo ya Zap ya Kampuni ya Zain Tanzania, Deo Tarimo, akizungumza katika hafla ya kutangaza wateja wa Kampuni ya Zain kununua petrol katika vituo vya mafuta vya kampuni hiyo kwa kutumia simu zao kupitia Zap, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zain Costantine Magavila na katikati ni Afisa wa Zain Praveena Lourens.


Mfanyabiashara wa visu vya kukunia Nazi, vinavyofanya shughuli zaidi ya moja, akionyesha jinsi visu hivyo vinavyofanya kazi ili kuwavutia wateja wake kama alivyokutwa na Sufianimafoto pembeni mwa Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, visu hivyo huuzwa kwa Sh. 1500 hadi 2000.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakichagua viatu kwa mchuuzi wa biashara hiyo jijini Dar es Salaam. Pamoja na agizo la Manispaa za jijini kuwataka wafanyabiashara hao kutopanga biashara zao pembezoni mwa barabara, agizo hilo linaonekana kupuuzwa kwani wafanyabiashara hao wamezidi kumiminika katika maeneo mbalimbali ya jijini na kuendelea na biashara zao.
Huu ndiyo msimu wa matunda kama unavyoona pichani ni Nanasi zikiwa zimejaa kwenye Soko la Buguruni Dar es Salam. Kwa sasa kila nanasi moja huuzwa kwa sh. 300, 500 hadi 1000.

Hii ni noma washkaji kukojoa mahali kama hapa hadhalani namna hii.......

Pamoja na jitihada za Manispaa ya Ilala kujenga vyoo katika Soko la Samaki la Kivukoni, Dar es Salaam ili kuepusha uchafuzi wa mazingira na magonjwa ya mlipuko, lakini bado baadhi ya watumiaji wa Soko hilo wanaonekana kupuuza utaratibu wa kutumia vyoo hivyo kama wanavyoonekana pichani wakijisaidia ndani ya Bahari ya Hindi katika eneo ambalo hutumiwa na baadhi ya wavuvi kusafishia samaki kabla ya kuingizwa Sokoni. Picha na (SPM)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.