Vijana wanaofanya shughuli zao katika Soko la samaki la Kivukoni Dar es Salaam, wakinyoana nywele kwa kutumia Wembe, ambao ni hatari kwa afya zao kutokana na kutumiwa kwa kazi hiyo kumnyoa mtu zaidi ya mmoja.
Askari wa Jiji wa Manispaa ya Ilala, wakivunja vibanda vya wafanyabiashara katika kituo cha daladala cha Akiba, ikiwa ni operesheni maalum ya kusafisha jiji na kuwaondoa wafanyabiashara katika vituo vya daladala jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili, wakiwa katika ziara ya kimasomo kukagua vyakula katika Soko la Nafaka la Kisutu Dar es Salaam jana. Wanafunzi hao watakuwa na ziara za kukagua vyakula katika masoko ya jijini, ambapo juzi walianza kukagua ubora wa samaki wanaouzwa katika Soko la Samaki la Kivukoni.
Wanafunzi hao wakikagua vyakula katika Soko la nafaka la Kisutu Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment