"Simu kama hii ndiyo iliyompatia Sh. milioni 13 Mariam wa Airport...jamani"
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Bidhaa za Reja reja Vodacom, Upendo Richard (katikati) na Mwakilishi wa Masoko Samsung Mobile, Amina Iddy (kulia) wakionyesha simu iliyokuwa ikishindaniwa katika Droo ya 'Ofa Bomba Samsung Promotion' wakati wa kuchezesha droo hiyo iliyochezeshwa Dar es Salaa jana. Kushoto ni Meneja Matukio na Promosheni wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa (nyuma), ni Msimamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao, ambapo Mkazi wa Airport jijini, Mariam Andwele, alijishindia kitita cha Sh milioni 13 baada ya kukunua simu ya Samsung na kuingizwa katika Droo hiyo. Picha Zote na (SPM)

Meneja Matukio na Promosheni wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha Droo ya 'Ofa Bomba Samsung Promotion', iliyochezeshwa Dar es Salaam jana ambapo Mkazi wa Uwanja wa Ndege jijini, Mariam Andwele, alijishindia kitita cha Sh milioni 13 baada ya kununua simu ya Samsung na kuingizwa katika Droo hiyo. (kushoto) ni msimamizi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha , Mrisho Millao, (kulia) ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mauzo ya bidhaa za reja reja wa Vodacom, Upendo Richard.
No comments:
Post a Comment