"Inabidi nasisi tuheshimike na kazi yetu bwana, wao walipokuwa Chuoni kusomea Uaskari, nasie tulikuwa Chuoni kusomea Kazi hii, ama jamani"...
Katibu Mkuu wa Chama cha Wapiga Picha za habari, ambaye pia ni Mpiga picha wa gazeti la Nipashe, Seleman Mpochi, akizungumza na waandishi kwenye uwanja wa ndege jana, kufafanua juu ya maamuzi yaliyopitishwa kwa pamoja ya waandishi ya kutoripoti ujio wa timu ya Taifa ya Ivory Cost, baada ya askari Polisi kuwanyanyasa, kuwasukuma na kuwapiga na virungu baadhi ya waandishi.
"Jamani tafadhalini naomba radhi kwa niaba yao, turudi tufanye kazi jamani msiondoke"...
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Jowel Bendera (katikati) na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Serengeti, Teddy Mapunda, wakiwa katikati ya kundi la waandishi wa habari wakiwatafadhalisha ili kurejea ndani ya geti la Uwanja wa Ndege wa mwalimu Julius Nyerere kuendelea na kazi ya kuripoti ujio wa timu ya Taifa ya Ivory Coast, iliyowasiri nchini mwishoni mwa wiki, baada ya waandishi kususia kuripoti ujio huo kwa kile kilichofanywa na askari kuwafukuza na kuwapiga virungu baadhi ya waandishi wakiwataka kuwa umbali wa mita 50 kutoka eneo watakalopita wachezaji wa timu hiyo. Picha zote na (SPM)

Waandishi wa habari wakitoka nje ya geti la Uwanja wa Ndege, baada ya kukubaliana kuondoka na kutoripoti ujio wa Ivory Coast, kwa kunyanyaswa na askari waliokuwa wakiwasukuma waandishi hao na kuwapiga virungu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Tanzania, Frederick Mwakalebela, akizungumza na waandishi kuwatafadhalisha kutoondoka mahala hapo na badala yake waendelee na kazi ya kuripoti tukio hilo, jambo ambalo halikukubaliwa na waandishi hao.

Hapa ni baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali, wakimweleza Mwakalebela kile walichotendewa na ambacho walishatendewa siku za nyuma kwa waandishi kupigwa virungu na askari polisi, na kama elimu haitatolewa kwa askari wetu basi matukio kama haya yataendelea siku hadi siku, kwani askari wengi wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kutaka sifa ili waonekane wanafanya kazi, na ili waonekane wanafanya kazi wao hudili zaidi na waandishi na wapiga picha pekee sasa sijui ni kwa vile hawa ndio huonekana zaidi ama la, na tusipoangalia na leo hii mambo haya yanaweza kutokea kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kirafiki baina ya Taifa Stars na Ivory Coast.

Huyu ndiye askari aliyekuwa na kisebusebu cha kuwafukuza waandishi tena kwa kauli chafu na kuwasukuma huku akizungusha fimbo yake aliyoishika mkononi, kutishia kuwapiga utazani alikuwa akifukuza ng'ombe waliokuwa wakila mazao.
No comments:
Post a Comment