"Huu msosi si mchezo babake, hivi Taswa nani mwingine hajaoa vile?.. nimekumbuka kumbe wengi, bado uhakika wa kula misosi kama hii upo oeni kila siku mtuite tufanye mambo", Siroooooooooooo! 
Hili ni jamaa fulani hivi linaitwa Ernest Mbozi, Beki wa timu ya Taswa Fc, inayoundwa na waandishi wa habari za michezo, likijipendelea kwa msosi wa nguvu ulioandaliwa na kamati makini ya sherehe ya harusi ya Amir Mhando na Mkewe Bi. Mariam, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha zZote na (SPM)

Saleh Ally (kulia) Ally Mkongwe na mkewe, wakipata msosi katika sherehe hiyo iliyofana, watu walikula na walipombeka babake usipime.

Huyu ni mpiga picha wa Gazeti la Habari leo, Mroki Mroki, akiwa na mkewe katika sherehe hiyo, ni mmoja kati ya watu wanaofanya kazi ofisi moja na Bwana harusi Amir Mhando.

Kushoto ni Sufianimafoto, na Issa Michuzi (nyuma) nao walikuwepo hapa wakipiga picha ya ukumbusho na bwana na bi harusi, ili kuweka mambo sawa ya kumbukumbu.

Hawa ni wafanyakazi wenzake na Amir Mhando, wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kutoa zawadi.

Issa Michuzi (mbele) mwenye kikofia cheupe, akiwaongoza wenzake kucheza mindoko ya muziki wa Nigerian, wakati wakienda kutoa zawadi.

Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Habari Leo, Amir Mhando (kushoto) akicheza na mke wake Mariam, wakati Mwanamuziki Ally Choki, alipokuwa akitoa burudani kwenye sherehe ya harusi yao.
No comments:
Post a Comment