Mmoja kati ya wasanii wa Luninga, akizungumza kuuliza maswali kuhusu maendeleo ya kijiji cha Wasanii kitakachojulikana kama 'Kijiji cha Wasanii' kitakachozinduliwa hivi karibuni huko Visegese Kisarawe, baada ya Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuanzisha umoja huo na kufikia jumla ya wasanii 400, hadi sasa ambao tayari ni wanachama watakaogaiwa maeneo hayo, Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam leo mchana.
Msanii wa vichekech 'Masanja', akihojiwa na waandihi wa habari baada ya kutoka kwenye Chumba hicho cha mkutano, akielezea furaha zake juu ya uanzishwaji wa kijiji hicho.
Baadhi ya wasanii wakiwa kwnye Chumba cha mkutano wakisikiliza kwa makini kuhusu taratibu za uzinduzi huo.
Wasanii wakongwe pia walikuwapo kuhakikisha yanayoelezwa na viongozi hao yatatekelezeka.
Huu ulikuwa ni muda wa msosi kila msanii alijisevia kiaina, kama unavyomuona JOTI, hakucheza mbali na muda ili kuwahi foleni ya maakuli, Ebwana eeh! kula muhimu babake!
Ebwana! kwenye kula hakuna mzaha wala ubrazameni, Dk Chain, akijipaki taratiiibu, pembezoni kusiko na bughuza.
"Huu ni muda wa msosi kwanza vichekesho baadaye bwana, hebu nipiche hiyo piga kwanza"
Huyu si mwingine ni Soud Ally, akitoka kujisevia msosi kama unavyomwona hana longolongo kwenye suala zima la makulaji.
No comments:
Post a Comment