Habari za Punde

*MKOA WA MARA KUTINGA MAHAKAMANI KUDAI HAKI,



Na Zaituni Kibwana, Jijini Dar es Salaam

BAADA ya kuondolewa kwenye mashindano ya Taifa hatua ya robo Fainali, Uongozi wa timu ya soka ya Mara imewasilisha rufaa kwenye shirikisho la soka la taifa TFF kupinga kuondolewa kwenye mashindano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa TFF Mwakalebela alisema Uongozi huo iliwasilisha rufaa hiyo jana kupinga kuondolewa katika mashindano hayo, hivyo tunatarajia kuunda kamati ambayo itaweza kusikiliza rufaa hivyo.
“Tumepokea pingamizi hilo ila tutaunda kamati ambayo itakuwa ni maalum ya kusikiliza kesi hiyo ambayo wanadai hawakutendewa haki ya kuondolewa kwenye mashindano hayo,”alisema.
Alisema wao kama TFF ni wajibu wao kufatilia malalamiko yote yanayotolewa na vilabu hivyo anawaomba uongozi huo kutokuwa na wasiwasi kwani rufaa yao ndio kwanza imekuaja jana ila itafanyiwa kazi na watajibiwa.
Timu hiyoimeondolewa kwenye mashindano hayo na TFF kwa kile walichodai kuwa katika mchezo wa Mey 8 kati ya Mara na Kilimanjaro katika uwanja wa Sheikh Abed jijini Arusha, Mkoa wao ulikiuka kanuni ya mashindano hayo kwa kumchezesha mchezaji Rudezi Kalinge, aliyesajiwa na klabu ya Polisi Morogoro kwa msimu wa 2009/2010 ambyo ilishiriki ligi daraja la kwanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.