Habari za Punde

*WASANII KUZINDUA KIJIJI CHAO, KUENDELEZA KILIMO KWANZA

Mmoja wa wasanii wa Luninga, akihoji maswali mbele kuhusiana na Maendeleo ya Kijiji cha Wasanii kinachotarajia kuzinduliwa hivi karibuni huko Visegeswe, Kisarawe, wakati wa mkutano wa maandalizi ya uzinduzi kijiji cha Wasanii, utakaojulikana kama 'Mji wa Wasanii',. Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dustan Mrutu, uliofanyika kwenye Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam leo mchana. ambapo watakaogaiwa maeneo hayo ni wasanii waliokwishajiunga na Shirikisho la Wasanii Tanzania(SHIWATA), ambapo tayari jumla ya wasanii 400, wamekwisha jiunga na kujihakikishia kupata maeneo hayo.

Baadhi ya wasanii wa Luninga na waigizaji wa filamu, wakiwa kwenye mkutano wa maandalizi ya uzinduzi wa Kijiji kipya cha Wasanii utakaojulikana kama Mji Mpya wa Wasanii. Mkutano huo ulifnguliwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dustan Mrutu, uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Vichekesho 'Komedi'. Masanja, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kutoka kwenye Chumba cha mkutano huo, akieleza yaliyomfurahisha kuhusiana na kijiji hicho cha wasanii.

"Kwanza msosi vichekesho baadae"
Huyu simwingine ni Soud Ally, akitoka kujisevia msosi, eti mwili haujengwi na matofali bali ni msosi pekee, si unamcheki katika mkono wa kushoto?

"Mapozi si katika uigizaji pekee hata katika kula pozi linahitajika usijetia aibu mzee mzima"
Dk Chain utazani anasubiri Take 2, ili kurekodi upya kipande chake, hapa haigizi mzee mzima bali alikuwa akijisevia makulaji wakati wa muda wa mapumziko wa mkutano huo.

Duh! Jamaa unanilenga mie tuuuu, unazani nitajaza zaidi ya hapa upate ya ukurasa wa mbele nini"?
Mchekeshaji wa KOMEDI, Joti kijisevia msosi utazani ananiliu.......

Wakongwe pia walikuwapo kuhakikisha masuala yote yanakwenda sawa, ili kufanikisha uzinduzi wa kijiji hicho.
Jamani eti hivi hawa wooote ni wasanii kweli? mboni huwa hatuwaoni katika Luninga zetu kama kinananiliu? ama ndo tayari wengine washapigiwa mapande nini?, eti pia ni wasanii wakiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.