Pamoja na bonge la party la kumuaga Heri Bomani, lakini pia ilikuwa ni siku maalum kwake iliyo na furaha na kumbukumbu ya kipekee, kwani pia alikuwa akitimiza miaka 'fulani hivi' kwahiyo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa hivyo aliua ndege wawili kwa jiwe moja.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Biashara (KCB), Heri Bomani, akikata Keki kuashiria sikukuu yake ya kuzaliwa aliyoiunganisha na sherehe ya kuagwa kwake na wafanyakazi wenzake wa benki hiyo iliyofanyika jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Kenya jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Biashara (KCB) Joram Kierie (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Janet Mbene, wakati wa sherehe ya kumaribisha Mwenyekiti huyo na kumuaga, aliyekuwa mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Heri Bomani, aliyeitumikia kwa miaka 4. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
"Asante sana Mama kwa zawadi hii"
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Janet Mbene, (kushoto) akimkabidhi Tuzo, aliyekuwa Mkurugenzi wa benki ya KCB, Heri Bomani, wakati wa sherehe ya kumaribisha Mwenyekiti huyo na kumuaga, Heri (katikati ) ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo, Joram Kierie.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa Heri Bomani.......
Heri Bomani, akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wa Benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Biashara (KCB) wakisebeneka na miondoko ya Afrika ya kusini wakati wa sherehe hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Biashara (KCB) wakisebeneka na miondoko ya Afrika ya kusini sambamba na Heri Bomani, wakati wa sherehe hiyo.
Hawa kama vile hawapo, wao wameketi mezani wakifuatilia sebene lililokuwa likimwagwa na wafanyakazi wenzao tuuuuuuuu.
No comments:
Post a Comment