Maandishi yenye ujumbe mahsusi yakiwa yameandikwa kwenye ukuta uliopo barabara ya Kawawa eneo la Karume Dar es Salaam. Maandishi hao yamekuwa yakiwashangaza walio wengi kutokana na ujumbe unaopatikana katika maandishi hayo kama lile linalosomeka ‘Kusoma kuelewa, Kukesha Mbwembwe tu’ .
*Njemba yauchapa usingizi ikiwa wima kwenye mlango wa daladala..
Kondakta wa daladala linalofanya safari zake Ubungo-Posta, ambaye hakuweza kufahamika jina lake, akiuchapa usingizi huku akiwa na pesa mkononi wakati gari hilo lokiwa kwenye mwendo katika foleni barabara ya Jangwani Dar es Salaam huku mlango ukiwa wazo. Jamani makondakta toeni Deiwaka basi ili mkapumzike fedha haina mwisho kila siku ipo tu hata ukilala ukaamka utaikuta hii ni noma.
*Mgambo wa jiji hebu waacheni hawa jamaa hata tu, yakula inapatikana hapa, mnapowachukulia vutu hivi mnavupeleka wapo????
Wafanyabiashara wa vitafunwa wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Posta Mpya Dar es Salaam jana wakisubiri wateja. Pamoja wa manispaa ya Ilala kuwaondoa wafanyabiashara hao lakini bado wanasongaana kituoni hapo kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa kituo hicho.
*Vijana wa Kinondoni 'B' wajikusanya na kutoa msaada kwa Yatima wa Chang'ombe Dar..
Kiongozi wa kikundi cha Umoja wa Vijana wa Kinondoni B, Dar es Salaam, Karama Ally (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada Juma Hamis (8) wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Hiyari Orphan Center Chang’ombe. Kikundi hicho cha Vijana kilifika kituoni hapo juzi na kutoa msaada wa Vitanda 3, unga na mikate. Wapili kushoto ni mmoja wa vijana wa kundi hilo, Patrick Thomas.
*Elimu kwa madereva ni muhimu, ajali za Treni na magari hutokea kwa uzembe wa madereva..
Pamoja na jitihada za kuwaelimisha madereva kutoegesha magari juu ya Reli pindi yanapokatiza kwenye Reli ili kuepuka kugongwa na Treni, lakini bado baadhi ya madereva wanahitaji elimu ya kutosha juu ya suala hilo, kama inavyoonekana pichani, Roli likiwa limesimama kwenye Reli katika foleni ya magari eneo la Tazara Buguruni Dar es Salaam.
*Dar hakitupwi kitu, hata Utumbo wa Mbuzi wa kuchoma dili...
Mfanyabiashara wa Utumbo wa Mbuzi wa kuchoma, ambaye hakupenda kutaja jina lake, akiandaa biashara hiyo katika mazingira yasiyofaa kwa mtumiaji kutokana na mazingira hayo eneo la Vingunguti Dar es Salaam jana, jambo ambalo linaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kwa watumiaji.
No comments:
Post a Comment