Habari za Punde

*MAISHA YA WAKAZI WA KIPAWA DAR BADO NI TATA

*Wacha tjenge tujishikize hadi kieleweke.....
Kijjana ambaye hakupenda kutaja jina lake akijenga banda kwa ajili ya kuisaidia familia yake ya Mzee Abdi Saleh (85) Mjumbe wa Shina Namba 13 CCM, (kulia) ikiwa ni jitihada za kujiifadhi mara baada ya kubomolewa nyumba zao Kipawa Dar es Salaam kwa ajili ya kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege. Wakazi hao wa Kipawa wameilalamikia serikali kwa kuthaminisha nyumba hizo miaka 13 iliyopita na kuwalipa baadhi yao mwaka huu jambo ambalo linawawia vigumu kujenga upya.
*Jamani tuelewane, itabidi tukasaini tu hata hicho kilichopo....kwanza..


Mwenyekiti wa wenyenyumba wa Kipawa, Magnus Mulisa, akizungumza na wenyenyumba waliobomolewa nyumb zao Kipawa waliofika kwenye Ofisi ya Mku wa Mkoa Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utaratibu wa malipo ya nyumba zao.
*Hatuna pa kwenda jamani malipo hayakidhi mahitaji ya ujenzi...



Abdi Saleh (85) Mjumbe wa Shina Namba 13 CCM, (kulia) ambaye ni mmoja kati ya watu waliovunjiwa nyumba zao Kipawa Dar es Salaam, akiwa na familia yake katika banda waliolojenga ili kujihifadhi baada ya kubomolewa nyumba yao. Wakazi hao wa Kipawa wameilalamikia serikali kwa kuthaminisha nyumba hizo miaka 13 iliyopita na kuwalipa baadhi yao mwaka huu jambo ambalo linawawia vigumu kujenga upya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.