Habari za Punde

*MAAJABU YA JIJI LA LUKUVI NA MATUKIO KADHAA

*Nabii wa Ajabu wa Karne ya 21 aibuka Dar, ahamasisha uzinzi, ulevi na yote yaliyokatazwa na maandiko matakatifu...

NABII WA KARNE YA 21
Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Nabii Tito, akiwahubiria wakazi wa jijini Dar es Salaam katikati ya Mitaa wa Posta, akiwahamasisha kuoa wanawake wengi, kunywa pombe, kula Kitimoto na kuzini akidai mambo hayo si dhambi bali ni maandiko matakatifu. Nabii huyo alimshangaza kila mmoja aliyepita eneo hilo na kupata wasaa wa kumsikiliza huku kila mmoja akiondoka mahala hapo akiangua kicheko wakati akitangaza katika kipaza sauti chake.
*Hawa mgambo sasa wanakera jamani, njaa zitawaua duh........

Askari wa Jiji, akiokota madumu ya maji yanayotumiwa na waosha magari na kuondoka nayo baada ya kuwafukuza vijana wanaofanya shughuli za kuosha magari kwenye Mtaa wa Ohia Dar es Salaam leo mchana.

*Hawa nao bila noma wanakokota maembe ya mshkaji sijui wanayapeleka wapi?????



Askari wa Jiji wa manispaa ya Ilala, wakikokota baiskeli ya mchuuzi wa matunda, baada ya kumnyang’anya wakati akifanya biashara hiyo kwenye Mtaa wa Samora Dar es Salaam. Askari hao walishatolewa tamko na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kutowanyang’anya wala kuwapiga biashara wafanyabiashara hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.