Habari za Punde

*BENKI YA CBA IMEPATA FAIDA YA Tshs 2.5bn KWA MWAKA 2009





Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Commercial (CBA), Nehemiah Kyando, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ripoti ya benki hiyo ya mwaka 2009. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Uzalishaji wa Benki hiyo, Aron Luhanga.
Na Sufianimafoto Ripoter, jijini
FAIDA hiyo ikiwa ni ongezeko la karibu Tshs 7bn kwa wanahisa kwa mwaka jana pekee. Kwa sasa CBA imeanza kufungua matawi kadhaa mikoani
Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Commercial Bank of Africa, Nehemiah Kyando, wakati alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
Aidha amesema kuwa kupata faida nono ya bilioni 2.5 kwa mwaka 2009 na kuonyesha kuwa ni benki imara inayojitoshereza kwa kuwa na mtaji wa kutosha.
Pamoja na mtikisiko wa dunia kiuchumi uliozikumba taasisi nyingi za fedha mwaka uliopita, benki hii imeendelea kukua na kujiimarisha.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja, mtaji wa CBA umekuwa kwa bilioni Tshs 57, au aslilimia 56, kutokana ongezeko la asilimia 67 la amana za wateja, kutoka Tshs 35 bilioni na kuwa Tshs 87.5 bilioni.
Mafanikio haya ni matunda ya bidii, busara na mikakati madhubuti ya CBA. Moja ya mikakati hiyo imekuwa ni kuweka kiasi cha mtaji wa Tshs 3.2 bilioni mwaka 2009 ili kusaidia mpango wake wa kukua na kupanuka. Matokeo kwa hakika yamekuwa ni ya kufurahisha – Msimamo wa muda mrefu wa benki, uwezo wa kubaini matatizo na kuchukua tahadhari mapema, uzingatiaji wa kanuni bora za kibenki – mtaji imara, sera za muda mrefu za kukopesha, na uwekezaji kwenye huduma kwa wateja imevutia wanahisa, ambao wameweezesha kuwa na ongezeko kifedha la kutoka Tshs 7.3 bilioni kwenda Tshs 14 bilioni.
Mafanikio hayaishii hapo tu. Kwa lengo la kuwa na wateja wengi na kuwafikia kwa urahisi zaidi, CBA hivi karibuni imefungua tawi jipya huko Mbeya na iko mbioni kufungua matawi mengine mapya manne; Kariakoo, Ohio Street (Dar es Salaam), Mwanza na Arusha. Makao makuu ya CBA pia yanahamia mtaa wa Ohio kwenye tawi jipa lilipo jingo jipya la Amani Place. Tawi linatarajiwa kuwa limeshaanza kufanya kazi ifikapo Februari 15, 2010.
“CBA tuko mstari wa mbele katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu wanaoongezeka kila siku na tunataraji kuzindua bidhaa mpya na utaratibu mpya wa kibenki ili kuendana na mahitaji ya wateja wetu” amesema Nehemiah Mchechu, Mtendaji Mkuu wa CBA, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kwa kuzingatia mkakati wake wa kuwa taasisi inayoongoza kwa kutoa huduma nzuri za kifedha, CBA inamalengo maalum ya kimasoko kwa wateja wadogo wadogo na wakubwa na imeungana na Umoja SWITCH ATM ambao wako katika hatua za mwisho za kusambaza kadi za ATM.
Kumekuwa na mwitikio wa ajabu. – mikopo imepanda kufikia asilimia 57, au Tshs 22 bilioni, kutoka 2008. mahitaji ya kukopesha yaenda sambamba na ukuaji wa mapato; mapato yanayotokana na riba yamepanda kwa asilimia 58 kutoka Tshs 6.7 bilioni kama ilivyoonyeshwa kwenye vitabu vya mwaka 2008 hadi Tshs 10.7 bilioni kwa kipindi kilichoishia 31 Desemba 2009.
Kwa ujumla, haya ni mafanikio ya kuridhisha kwa benki ambayo imeendelea kuimarika kutokana mafanikio ya kipindi kilichopita. Kuanzia 2007 ambapo faida isiyolipiwa ushuru ilikuwa Tshs 215 milioni, 2008 Tshs 1.4 bilioni, 2009 Tshs 2.5.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.