Habari za Punde

*MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA, YAWAACHIA HURU FRANCIS NGUZA NA NGUZA MBANGU, YAWAFUNGA MAISHA PAPII KOCHA NA NGUZA VIKING 'BABU SEYA'

Na Sufianimafoto Ripoter, jijini
ILIKUWA ni kilioa na nyuso zilizojawa na huzuni tele miongoni mwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa Familia ya mwanamuziki Nguza Viking, waliofika kwenye Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam leo mchana pale Mahakama hiyo ilipowaachia huru Francis Nguza na Nguza Mashine na kuwafunga kifungo cha Maisha Papii Kocha na Nguza Viking.

Vilisikika vilio Mahakamani hapo mara tu, Jaji alipomaliza kusoma hukumu yake iliyowataja Nguza na Papii kuendelea kutumiakia kifungo cha maisha, huku kila mmoja akilia na kutamani kuwashika angalau mikono wanamuziki hao bila mafanikia kutokana na kuwa chini ya ulinzi wa Askari Magereza.

Kilio kilichowahuzunisha zaidi watu waliokuwapo Mahakamani hapo ni kile cha Mtoto Francis, aliyelia kwa huzuni kubwa na sauti kubwa Mahakamani hapo akiwasikitikia Baba yake na Kaka yake waliotajwa kuwa wanaendelea kutumikia kifungo cha maisha huku Mwanasheria wao Marando akiwapa pole na kumtaka Francis kunyamaza akimwambia “sasa utaendelea na masomo yako”.

Naye Papii Kocha wakati akitoka Mahakamani hapo alipunga mkono kwa watu lukuki waliokuwapo Mahakamani hapo huku akisema “HAKUNA MWINGINE, SASA ATATUOKOA JK”


*Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika Mahakama ya Rufaa leo Kesi ya Babu Seya....



Papii Kocha akianza kushuka katika gari la Magereza mara baada ya kuwasili kwenye Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam Tanzania leo asubuhi.



Babu Seya (katikati) akiwa na mwanae Papii Kocha wakiwa wamefungwa pingu mara baada ya kutelemka kwenye gari hilo.


















Nguza na wanae wakiingia kwenye Mahakama ya Rufaa leo asubuhi.




Nguza "Babu Seya' (kushoto) akiwa na wanae, Papii Kocha, Nguza Mashine na Francis Nguza wakiwa kwenye Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam Tanzania leo wakati wakisubiri kusomewa hukumu ya kesi yao, ambayo iliwatia hatiani Babu Seya na Papii Kocha kwa kuwafunga maisha na kuwaachia huru, Francis Nguza na Nguza Mbangu.
*"Pole sana kijana sasa utaendelea na masomo yako kama kawaida usijali"..









Wakili wa kujitegemea, Mabere Marando (kulia) akiwapongeza na Nguza Mbangu Francis Nguza (kushoto), walioachiwa huru na Mahakama ya Rufaa Tanzania, mara baada ya hukumu yao leo na kuwatia hatiani, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Papii Nguza kwa makosa ya ubakaji.

*"Usijali mwanangu tuombe mungu, hukumu imeamua tumebaki wawili"...








Babu Seya (kulia) akikumbatiana na mwanaye Papii Nguza baada ya kusomewa hukumu yao.
*"Usilie mdogo wangu yote maisha tu nyamaza, usijali kapige kitabu mungu atakusaidia utasahau"......








Papii Nguza (wapili kulia) akimfuta machozi mdogo wake Francis Nguza (kushoto) aliyekuwa akilia baada ya kusomewa hukumu iliyowatia hatiani, Nguza Viking ‘Babu Seya’ (kulia) na Papii, na kuwaachia huru Nguza Mbangu (wapili kushoto) na Francis, katika Mahakama ya Rufaa Tanzania Dar es Salaam.
"Jamani ntaishije mie Mtaani bila Baba, Kaka wala nyumba mie"







Francis Nguza akilia kwa uchungu mara baada ya kusomewa hukumu yao.









Francis.......









Waandishi wa habari wakiwazonga wanafamilia hao mara baada ya hukumu.
"Hebu sogeeni huko hawa bado wako chini yetu"









Haya sasa sogeeni tuachieni njia tupite hawa bado si raia bado wapo chini yetu.
"Jamani msijali sasa atakayetusaidia ni Rais Jakaya Kikwete Pekee"









Papii Kocha akitoka kwenye chumba cha Mahakama hiyo huku akiwa chini ya ulinzi, akisema anaamini Rais Jakaya Kikwete pekee kwa sasa ndiye mwenye uwezo wa kuwasaidia kwa hatua hiyo waliyofikia.









Ndugu wa Familia ya Nguza Viking, wakiangua kilio nje ya Mahakama ya Rufaa Tanzania Dar es Salaam, mara baada ya Familia hiyo kusomewa hukumu na leo.








Huyu ni Shangazi wa familia huyo, Mwisa Matuka Bizoo, akiangua kilio kwa uchungu nje ya Mahakama hiyo.








Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, waliojitokeza kusikiliza kesi hiyo leo, wakiwa nje ya Mahakama hiyo








Baadhi ya waandishi wa habari na Wakazi wa jijini wakitoka kwenye lango kuu la Mahakama ya Rufaa baada ya kesi hiyo kusomewa hukumu.
" He kumbe wanatokea mlango wa nyuma duh! tumepogwa bao na kina Khalfani na Badi, kumbe ndo maana waliondoka kimyakimya sijui tutawawahi"????????









Baadhi ya waandishi wa habari wakitimua mbio kuwawahi wakina Nguza wakati wakipanda gari la magereza mara baada ya kupitishiwa mlango wa nyuma.
"Haya weeee tumechelewa wameshapanda gari haooo wanaondoka".....









Wapiga pocha wa magazeti tofauti wakipiga picha gari lililowabeba kina Babu Seya.










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.