Meneja Mkuu wa Uhusiano, Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Serengeti, Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchna, wakati akitangaza uzinduzi wa kampeni ya 'Funga Goli' Kanda ya Ziwa, kuelekea mchezo wa kirafiki baina ya Taifa Stars na The Cranes ya Uganda utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza tarehe 3/3/2010.
Na Sufianimafoto Reporter
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua ya ‘Funga Goli’ Kanda ya Ziwa, lengo likiwa ni kuhamasisha mshikamano wa watanzania kwa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ kuelekea mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Uhusiano, Habari na Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda, amebainisha kuwa raha ya mchezo wa soka ni kufunga magoli ama ushindi. Hivyo amewataka wapenzi wa soka wa mkoani Mwanza na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa ili kuiwezesha kupata ushindi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Uhusiano, Habari na Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda, amebainisha kuwa raha ya mchezo wa soka ni kufunga magoli ama ushindi. Hivyo amewataka wapenzi wa soka wa mkoani Mwanza na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa ili kuiwezesha kupata ushindi.
Kampuni ya bia ya Serengeti, ambao ndio wadhamini wakubwa wa ‘Taifa Stars’ mpaka ifikapo mwaka 2011 wakati huu wataendesha kampeni hiyo maalumu ijulikanayo kama ‘Funga Goli’ katika mkoa wa mwanza.
Mapunda ametoa wito kwa wakazi wa Mwanza kutembelea katika baa za karibu ili kushiriki katika kampeni hiyo na kupata fursa ya kuwa miongoni mwa washindi watakaojinyakulia zawadi mbalimbali. Miongoni mwa zawadi hizo ni fulana, kofia, bia pamoja na kujishindia tiketi ya kushuhudia mchezo huo baina ya Taifa Stars na The Cranes katika uwanja wa Kirumba utakaopigwa tarehe 3 Machi 2010.
Siku wa mchezo huo wa soka, kutakuwa na maandamano ya barabarani (Road Show) katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza na yataishia katika uwanja wa soka wa Kirumba.
Kampeni hii inazinduliwa kwa mara ya kwanza kanda ya ziwa katika jitihada ya kuiunga mkono Taifa Stars. Kampuni ya bia ya Serengeti inawatakia kila la kheri watanzania wote kuishangilia na kuiunga mkono timu yetu.
No comments:
Post a Comment