Habari za Punde

*59 WAJITOKEZA KUOMBA KUMRITHI MAXIMO, 49 NI KUTOKA ULAYA










Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Leodgar Tenga, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu, mchakato wa kumpata mrithi wa Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), ambapo hadi sasa jumla ya watu 59 wameshajitokeza kuwania nafasi hiyo, 48 kati yao ni kutoka Mataifa ya Ulaya. Katikati ni Meneja Mkuu wa Habari, Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia Serengeti, Teddy Mapunda na Mkurugenzi wa Kampuni ya CXC, Africa, Charles Hamkah.



Na Sufianimafoto Reporter, jijini
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodger Tenga, alisema kuwa mpaka sasa jumla ya watu 59, wamekwishatuma maombi ya kuomba nafasi hiyo anayotarajia kuiacha Kocha Mkuu wa taifa Stars, Marcio Maximo, ambapo 49, kati yao ni kutoka Mataifa ya Ulaya.
Na kuongeza kuwa 3 ni wazawa, 3 kutoka nchi za Africa, 3 kutoka Asia na 2 kutoka South America, ambapo alizitaja sifa za wagombea hao kuwa ni awe na Diproma ya Koach, awe na angalau elimu ya kidato cha nne, na pia awe na uwezo wa kuwafundisha makocha.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.